Lugha Nyingine
UN yateua wanasayansi wawili wa China katika Jopo Huru la Kisayansi la Kimataifa juu ya AI
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeteua wajumbe 40 kutoka nchi mbalimbali, wakiwemo wawili kutoka China katika Jopo Huru la Kisayansi la Kimataifa juu ya Akili Mnemba (AI) ambapo ujumbe wao utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Februari 12, 2026 hadi Februari 11, 2029.
Wanasayansi hao wawili wa China walioteuliwa ni Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa AI ya Shanghai, Song Haitao, na Mwanataaluma katika Akademia ya Uhandisi ya China na mtaalamu wa teknolojia ya kompyuta ya wingu Wang Jian.
Katika taarifa yake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema uteuzi huo "unaashiria hatua ya msingi kuelekea uelewa wa kisayansi wa AI duniani.
“Katika dunia ambayo AI inakwenda kwa kasi zaidi yetu, jopo hili litaleta kile ambacho kimekuwa kikikosekana ---maarifa makini, huru ya kisayansi ambayo yatawezesha nchi wanachama, bila kujali uwezo wao wa kiteknolojia, kushiriki katika mijadala kwa usawa” amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



