Ushirikiano kati ya China na Afrika waelezwa kuweza kuongeza kasi ya mageuzi ya teknolojia ya uchimbaji madini Afrika

(CRI Online) Februari 13, 2026

Wawakilishi wa kampuni za China na za kimataifa kwenye Mkutano wa Uwekezaji katika Uchimbaji Madini Afrika Indaba 2026 wamesema, ushirikiano wa China na Afrika unaweza kuongeza kasi ya mageuzi ya kiteknolojia katika sekta ya uchimbaji madini ya Afrika.

Katika mkutano huo uliofanyika Cape Town, wajumbe hao wakirejelea kuwa utaalamu, suluhu za kijani za China na uhusiano wa kiviwanda kuwa ni viwezeshaji muhimu.

Mkutano huo ulioanza Jumatatu wiki hii na kumalizika jana Alhamisi katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Cape Town, ulikutanisha wajumbe zaidi ya 10,500 kutoka ndani na nje ya Afrika.

Wajumbe hao wamesema, ushirikiano wa karibu zaidi kati ya China na Afrika unaweza kuongeza kasi ya mageuzi katika sekta ya uchimbaji madini, hususan katika maeneo kama vyombo vya kujiendesha vyenyewe, masuala ya kidijitali, na maendeleo ya kijani.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha