Mkutano wa Baraza Tendaji la AU wafunguliwa, ukifuatilia usalama wa maji, mshikamano na amani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 12, 2026

Picha hii iliyopigwa Februari 11, 2026 ikionyesha ukumbi wa Mkutano wa 48 wa Kawaida wa Baraza Tendaji la Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Xie Jianfei)

ADDIS ABABA – Mkutano wa 48 wa Kawaida wa Baraza Tendaji la Umoja wa Afrika (AU) umeanza rasmi jana Jumatano katika makao makuu ya AU huko Addis Ababa, Ethiopia.

Mkutano huo wa siku mbili, unaohudhuriwa na mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi wanachama wa AU chini ya mfumo wa Mkutano wa 39 wa Viongozi AU, unafanyika chini ya kaulimbiu ya AU ya 2026: "Kuhakikisha Upatikanaji Endelevu wa Maji na Mifumo Salama ya Usafi wa Mazingira ili Kufikia Malengo ya Ajenda ya 2063."

Akihutubia kikao cha ufunguzi, Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU Mahmoud Ali Youssouf ameelezea masuala muhimu ya bara hilo ambayo yanatakiwa kuzingatiwa na mawaziri hao wa mambo ya nje.

Amesisitiza kuchukulia maliasili ya maji na usafi wa mazingira kuwa ni mada ya mwaka, kuimarisha nafasi na mshikamano wa Afrika kwenye jukwaa la kimataifa, na kuhimiza amani na utulivu kote barani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Gedion Timothewos amesema katika hotuba yake kwamba wajumbe wanapokusanyika kwenye mkutano huo chini ya mwavuli wa umoja huo, ambao ulianzishwa kwa madhumuni ya kufikia uhuru wa kisiasa na mafungamano ya kiuchumi, wanakumbuka umuhimu wa mshikamano kwa usalama, uhuru, na ustawi wa pamoja."

Mkutano huo wa Baraza Tendaji unatarajiwa kupitia mswada wa ajenda na maamuzi ya Mkutano wa 39 wa Kawaida wa Baraza la Wakuu wa Nchi na Serikali la AU, uliopangwa kufanyika Februari 14-15.

Taarifa iliyotolewa na AU inasema mawaziri hao wa mambo ya nje wa Afrika pia watajadili ushiriki wa umoja huo katika Kundi la 20, kufanya uchaguzi na uteuzi katika vyombo na taasisi za AU, kupitia utekelezaji wa maazimio yaliyotolewa na Baraza Tendaji, vilevile kuzingatia mswada wa nyaraka za sheria na masuala ya uongozi wa kitaasisi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Gedion Timothewos akizungumza kwenye Mkutano wa 48 wa Kawaida wa Baraza Tendaji la Umoja wa Afrika (AU) kwenye makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, Ethiopia, Februari 11, 2026. (Xinhua/Geng Xinning)

Picha hii iliyopigwa Februari 11, 2026 ikionyesha makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Xie Jianfei)

Picha hii iliyopigwa Februari 11, 2026 ikionyesha makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Xie Jianfei)

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mahamoud Ali Youssouf akizungumza kwenye Mkutano wa 48 wa Kawaida wa Baraza Tendaji la Umoja wa Afrika (AU) kwenye makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, Ethiopia, Februari 11, 2026. (Xinhua/Geng Xinning)

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika (UNECA) Claver Gatete akizungumza kwenye Mkutano wa 48 wa Kawaida wa Baraza Tendaji la Umoja wa Afrika (AU) kwenye makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, Ethiopia, Februari 11, 2026. (Xinhua/Geng Xinning)

Picha hii iliyopigwa Februari 11, 2026 ikionyesha ukumbi wa Mkutano wa 48 wa Kawaida wa Baraza Tendaji la Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Geng Xinning)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha