Rais Xi atoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi kwa maofisa na askari wa majeshi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 12, 2026

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiwapungia mkono maofisa na askari wa majeshi kupitia njia ya video mjini Beijing, Februari 10, 2026. (Xinhua/Li Gang)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping Jumanne wiki hii alikagua utayari wa kupigana vita wa vikosi vya majeshi na operesheni zinazoendelea na kutoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa maofisa na askari wote wa nchini kwa njia ya video mjini Beijing.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiwa kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama na Kamati Kuu ya Kijeshi ametoa salamu za dhati kwa maofisa na askari wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na Jeshi la Polisi la China, wafanyakazi wa kiraia wanaofanya kazi majeshini, pamoja na maofisa na askari wa vikosi vya akiba na wanamgambo.

Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China itaanzia tarehe 17 mwezi huu.

Rais Xi alizungumza kwa njia ya video na vikosi tisa kutoka majeshi tofauti ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China na Jeshi la Polisi, na kuwapongeza kwa utendaji wao mzuri katika majukumu yao husika.

Akiuelezea mwaka uliopita kuwa usio wa kawaida na maalum, Rais Xi amesema vikosi hivyo vya umma vimehimiza marekebisho ya kisiasa kwa kina, kukabiliana kithabiti na hatari na changamoto mbalimbali, na kupitia "mapinduzi makali" katika mapambano dhidi ya ufisadi.

Rais Xi amesema maofisa na askari katika vikosi vyote vya majeshi, hasa wale wa mashinani, wamekuwa waaminifu kwa Chama, wametimiza majukumu yao kwa uaminifu, na wamethibitishwa kuwa ni wenye uwezo na wa kutegemewa.

"Kudumisha utayari wa kupigana vita wakati wa siku za mapumziko ni desturi nzuri ya vikosi vyetu vya majeshi," Rais Xi amesema, akilihimiza jeshi kukaa macho na kulinda usalama wa nchi na ustawi wa watu.

Vikosi tisa kutoka majeshi tofauti ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na Jeshi la Polisi la China vikiripoti kwa video kwa Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), Februari 10, 2026. (Xinhua/Li Gang)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha