Botswana kuimarisha nidhamu ya matumizi wakati wa kukabiliwa na changamoto za mambo ya fedha

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 11, 2026

GABORONE - Serikali ya Botswana itatekeleza mageuzi ya mfumo na kuimarisha hatua za nidhamu ya matumizi ya fedha kutokana na kuongezeka kwa deni la kiumma katika mwaka ujao wa fedha utakaoanzia mwezi Aprili.

Akitoa hotuba ya bajeti ya 2026/2027 katika Bunge la Taifa mjini Gaborone siku ya Jumatatu, Makamu Rais ambaye pia ni Waziri wa Fedha wa Botswana Ndaba Gaolathe amebainisha kazi zinazopewa vipaumbele vya kitaifa zikiwa ni pamoja na kuongeza mauzo ya nje na kukuza uchumi wa aina mbalimbali, na hayo yote yanaendana na Mpango wa 12 wa Maendeleo ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika na Mpango wa kubadilisha muundo wa uchumi wa Botswana, yakilenga kupunguza hali ya kutegemea almasi kwa kupita kiasi.

“Kilimo kinabadilishwa kutoka hali ya kujikimu na kutegemea uagizaji kutoka nje hadi kuwa sekta ya kisasa ya kilimo na viwanda inayolenga mauzo ya nje inayojengwa juu ya minyororo ya thamani, utengenezaji wa mazao ya kilimo, na ufikiaji wa soko la kikanda na kimataifa” Gaolathe amesema.

Pia amesisitiza ushiriki wa mashirika binafsi ni kiini cha injini endeshi kwa kuongeza nguvu ya ushindani na kuharakisha ukuaji endelevu.

Kuhusu huduma ya afya, waziri huyo ametoa wito wa kuanzishwa kwa huduma za uhakikishaji wa matibabu kwa wananchi wote wa Botswana kwa kupitia kuzifanyia mageuzi idara za afya, na inatarajiwa kupunguza matumizi ya serikali ya kununua zana na vifaa vya tiba kwa asilimia 30 hadi asilimia 40 ndani ya miaka mitano.

“Nakisi zinazoendelea na mapato yanayoshuka vimepunguza akaunti ya uwekezaji ya serikali hadi kiwango cha chini zaidi na kisicho cha endelevu katika historia," Gaolathe amesema.

Amesisitiza kuwa, katika mwaka ujao wa fedha, serikali itachukua hatua za kuunganisha kazi za kifedha, kuimarisha nidhamu ya matumizi, na kujenga upya bafa ya kupunguza athari kwa mambo ya fedha ili kuimarisha uendelevu wa deni na kurejesha uhimilivu wa kiuchumi.

Matumizi ya serikali ya Botswana yamekadiriwa kuwa pula bilioni 103.58 (dola za Marekan takribani bilioni 7.88), dhidi ya mapato ya pula bilioni 77.22. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha