Lugha Nyingine
Trump ataka Marekani itupie macho mbele baada ya kutolewa kwa nyaraka za Epstein huku Baraza la Wawakilishi likidai majibu

Rais wa Marekani Donald Trump akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, Washington, D.C., Marekani, Januari 20, 2026. (Picha na Li Yuanqing/Xinhua)
WASHINGTON - Rais wa Marekani Donald Trump anataka Marekani itupie macho mbele baada ya kutolewa kwa nyaraka mfululizo kuhusu mlawiti aliyekubuhu zaidi duniani Jeffrey Epstein lakini bunge la taifa la Marekani na manusura wanaendelea kudai majibu.
Miezi ya hivi karibuni Wizara ya Sheria ya Marekani (DOJ)imetoa mamilioni ya nyaraka kuhusu uchunguzi wake wa Jeffrey Epstein, ambaye alikamatwa mwaka 2019 kwa mashtaka ya biashara haramu ya ngono lakini baadaye alifariki gerezani kabla ya kufikishwa mahakamani.
"Nadhani hivi sasa kweli ni wakati kwa nchi yetu kufuatilia lazima mambo mengine," Trump hivi karibuni aliwaambia waandishi wa habari katika Ofisi ya Oval.
Alhamisi asubuhi wiki iliyopita Baraza la Seneti linaloongozwa na chama cha Republican lilikataa ombi kutoka kwa Kiongozi wa Wabunge walio wachache wa Democrat Chuck Schumer la kuishtaki serikali ya Trump kwa jinsi ilivyoshughulikia kutolewa kwa nyaraka hizo za Epstein.
Kiongozi huyo wa wabunge wa Democrat alisema Ikulu ya White House haifuati sheria iliyopitishwa kwenye bunge la taifa mwaka jana, sheria ambayo iliitaka Wizara ya Sheria kutoa nyaraka zote zinazohusu uchunguzi wake juu ya Epstein.
Schumer aliishutumu Wizara ya Sheria kwa kushindwa kuweka haradhani nyaraka zote muhimu.
Naibu waziri wa sheria wa Marekani Todd Blanche alisema serikali imekamilisha upitiaji wake wa nyaraka hizo, kwa mujibu wa sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la taifa mwezi Novemba. Blanche alisema hakuna sababu za kutoa mashtaka mapya.
"Kuna mawasiliano ya barua nyingi, pamoja na barua pepe nyingi, na pia kuna picha nyingi. Lakini hayo yote huenda hayaturuhusu tumshtaki mtu fulani." Blanche alisema hivi karibuni.

Picha hii iliyopigwa Oktoba 21, 2025 ikionyesha jengo la Bunge la Marekani, Capitol, Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Li Rui)
Hata hivyo, Baraza la Wawakilishi linaendelea na uchunguzi wake.
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Hillary Clinton wanatakiwa kutoa ushahidi mbele ya bunge la taifa siku za baadaye mwezi huu, kabla ya hapo Wabunge wa Republican kutishia kuwawajibisha kwa kudharau bunge la taifa kama hawatajitokeza.
Bill Clinton alikuwa akimfahamu Epstein, lakini anakanusha kujua kuhusu makosa yake ya ngono, na anasema alikata mawasiliano naye miongo miwili iliyopita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



