Lugha Nyingine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi kwa Wachina

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akitoa salamu kupitia njia video katika sherehe ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Februari 9, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa Wachina.
Katika hafla ya kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China iliyoandaliwa na ujumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, Bw. Guterres ameishukuru China na wananchi wake kwa kuunga mkono ushirikiano wa pande nyingi na mshikamano wa dunia.
“Tunapokaribisha Mwaka Mpya wa Farasi, tunasherehekea alama hiyo ya nguvu, mafanikio na ujasiri wa kusonga mbele--- sifa ambazo dunia yetu inazihitaji sana, tunapokabiliana na migogoro, ukosefu wa usawa na janga la mabadiliko ya tabianchi.” Guterres amesema katika ujumbe wake kwa njia ya video kwenye sherehe hiyo.
Ametoa wito wa kuendelea kujitolea kwa pamoja kwa amani, heshima na maendeleo endelevu kwa wote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



