Lugha Nyingine
Idadi ya abiria na kiasi cha mizigo katika reli ya SGR ya Kenya vyafikia rekodi ya juu mwaka 2025
(CRI Online) Februari 11, 2026
Reli ya SGR ya Kenya imerekodi ongezeko linalovunja rekodi la abiria na kiasi cha mizigo katika mwaka 2025 wakati mahitaji yakiongezeka.
Mamlaka ya Taifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS) imetangaza Jumatatu wiki hii kwamba, idadi ya abiria katika reli hiyo iliyojengwa na China imefikia milioni 2.73 mpaka kufikia mwisho wa mwaka jana, ikiwa ni ongezeko kutoka abiria milioni 2.44 waliorekodiwa mwaka 2024.
Mahitaji makubwa ya huduma ya treni za abiria yamelifanya Shirika la Reli la Kenya (KR) mara kwa mara kuongeza treni za ziada.
Kiasi cha mizigo kilichosafirishwa na treni hiyo mwaka 2025 kiliongezeka na kufikia tani milioni 7.48, ambayo ni ongezeko kutoka tani milioni 6.53 zilizosafirishwa mwaka 2024.
(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



