Lugha Nyingine
Viongozi wa Tanzania na Uganda waahidi kuboresha uhusiano wa pande mbili na ushirikiano wa kikanda

(Xinhua/Emmanuel Herman)
Viongozi wa Tanzania na Uganda wameahidi kuboresha uhusiano wa pande mbili na ushirikiano wa kikanda wakati wa ziara ya rais wa Uganda Yoweri Museveni nchini Tanzania.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na rais Museveni walirejea tena uhusiano wa kihistoria kati ya nchi hizo mbili na kutoa wito wa kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya pamoja, ukiwemo mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).
Viongozi hao wamekubaliana kuboresha miundombinu ya usafiri katika Ziwa Viktoria na kuboresha ufanisi wa biashara kupitia bandari za Dar es Salaam na Tanga, na pia waliahidi kuondoa vizuizi visivyo vya kiushuru na kuboresha mazingira ya biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

(Xinhua/Emmanuel Herman)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



