Lugha Nyingine
Zimbabwe yatarajia uhusiano imara zaidi wa kiuchumi na China
(CRI Online) Februari 09, 2026
Waziri wa Masuala ya Wanawake, Jamii, na Maendeleo ya Viwanda Vidogo na vya Kati wa Zimbabwe, Monica Mutsvangwa amesema, uhusiano wa kiuchumi kati ya China na Zimbabwe unatarajiwa kupata kasi mpya wakati ushirikiano wa pande hizo mbili ukiendelea kupanuka.
Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua, Mutsvangwa amesema, viwanda vidogo na vya ukubwa wa kati vitaimarisha zaidi ushindani wao kupitia kuongezeka kwa upatikanaji wa soko, uhamishaji wa teknolojia na uwekezaji katika mwaka ujao.
Amesema uhusiano kati ya Zimbabwe na China umejikita katika uungaji mkono wa kihistoria wa China kwa Zimbabwe wakati ikitafuta uhuru wake, na sasa unaendelea na kuwa uhusiano wa kisasa unaolenga ustawi wa pamoja.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



