Lugha Nyingine
Uganda yafanya tamasha la kusherehekea mawasiliano ya watu na watu wakati Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ikikaribia
Uganda imezindua Mwaka wa Mawasiliano ya Watu na Watu kati ya China na Uganda wakati wa tamasha lililofanyika mjini Kampala, mji mkuu wa Uganda hapo jana Jumapili, kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Makamu wa rais wa Uganda Jessica Alupo amesema ushirikiano kati ya China na Uganda umekuwa ni wa kunufaishana, na kuishukuru China kwa kuunga mkono maendeleo ya miundombinu nchini Uganda, ufadhili wa masomo, na miradi ya kujenga uwezo. Amesema mawasiliano kati ya watu na watu yanatengeneza msingi imara wa uhusiano wa kudumu, akisema Afrika na China zimeutangaza mwaka 2026 kuwa Mwaka wa Mawasiliano ya Watu na Watu kati ya China na Afrika.
Naye Kaimu Balozi wa China nchini Uganda, Fan Xuecheng amesema, tamasha la Mwaka Mpya wa Jadi wa China ni sikukuu muhimu ya jadi kwa watu wa China, na sherehe kama hizo zinazofanyika kwenye mahekalu zinaakisi kuwa watu ni msingi wa ushirikiano kati ya China na Uganda.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



