Afrika Kusini yaamua kuondoa kikosi chake kutoka ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC

(CRI Online) Februari 09, 2026

Ikulu ya Afrika Kusini jana Jumapili imetoa taarifa ikisema kuwa, nchi hiyo imeamua kuondoa kikosi chake kutoka ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO).

Taarifa hiyo imesema, rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alimwarifu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres uamuzi huo wakati wa mazungumzo ya simu yaliyofanyika tarehe 12 mwezi Januari, ambapo alisema uamuzi huo ulifanyika kwa mujibu wa mahitaji ya Afrika Kusini kuhusu kupanga upya rasilimali za jeshi lake. Pia rais Ramaphosa alisema, Afrika Kusini itashirikiana kwa karibu na Umoja wa Mataifa ili kuhakikisha mchakato wa kuondoka kwa utaratibu na kwa uwajibikaji, na inatarajiwa kukamilisha zoezi hilo kabla ya mwisho wa mwaka 2026.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha