Lugha Nyingine
Shukrani za juu kabisa: Mama mtanzania ampa mtoto wake jina la daktari Mchina aliyemwokoa
Liu Huiling (kushoto) akipiga picha na Salma Kombo Omar, ambaye anabeba mtoto wake, visiwani Zanzibar, Tanzania, Januari 14, 2026. (Kundi la 35 la Timu ya Madaktari Wachina visiwani Zanzibar/kupitia Xinhua)
ZANZIBAR, Tanzania – Ndani ya wodi nyeupe za Hospitali ya Abdulla Mzee katika Kisiwa cha Pemba cha Zanzibar, Tanzania, simulizi tulivu lakini yenye nguvu kuhusu maisha, shukrani, na urafiki wa kuvuka mipaka imeota mizizi.
Mtoto mchanga wa kike Mtanzania, aliyebebwa kwa upole mikononi mwa mama yake, amepewa jina la Kichina "Liu" ambalo linasimulia chanzo cha simulizi hiyo.
Mtoto huyo amepewa jina hilo kumenzi Liu Huiling, daktari Mchina ambaye maamuzi yake ya haraka na kujitolea kwake bila kuyumba yaliokoa maisha ya mama wa mtoto huyo, Salma Kombo Omar, aliyepata mshtuko wa septiki (septic shock) baada ya kujifungua kwa upasuaji.
Tukio hilo lilishughulikiwa na daktari wa kundi la 35 la timu ya madaktari Wachina visiwani Zanzibar, ambapo uingiliaji wao wa haraka uliigeuza dharura iliyokaribia kusababisha kifo kuwa simulizi ya matumaini.
Kwa mujibu wa Omar, masaibu hayo yalianza mwezi mmoja mapema, alipokimbizwa Hospitali ya Abdulla Mzee siku 20 baada ya kujifungua. Maambukizi makali ya ndani ya tumbo yalizuka na kuongezeka kwa kasi hadi kufikia mshtuko wa septiki.
Alipofikishwa hospitalini, shinikizo lake la damu lilikuwa limeshuka hadi kiwango cha hatari, dalili muhimu hazikuwa thabiti, na alikuwa katika hali ya nusu fahamu. Madaktari waligundua mkusanyiko mkubwa wa mate ya uvimbe tumboni mwake, na kumweka katika hatari ya kufeli kwa viungo vingi vya mwili.
"Hakukuwa na nafasi ya kusitasita. Kila sekunde ilikuwa ni mbio dhidi ya kifo," alikumbushia Liu Huiling, kutoka Hospitali ya Pili ya Lianyungang, mashariki mwa China.
Ndani ya chumba cha upasuaji, ukubwa wa maambukizi ulidhihirika dhahiri: pus ilikuwa imeenea kwa kiasi kikubwa, zaidi ya matarajio ya awali.
Chini ya mazingira makali ya usafi wa kitabibu, Liu alifanya uchunguzi wa kina huku Zhu Shuangjiu, daktari mwingine kutoka timu hiyo ya madaktari, akitoa mwongozo thabiti. Hata hivyo, hatua ya kupona ikawa changamoto nyingine.
Liu Huiling (kushoto) akipiga picha na Salma Kombo Omar (wa pili kulia) pamoja na wauguzi, visiwani Zanzibar, Tanzania, Januari 14, 2026. (Kundi la 35 la Timu ya Madaktari Wachina visiwani Zanzibar/kupitia Xinhua)
Utunzaji wa jeraha wa kila siku ukawa sehemu ya utaratibu wa Daktari Liu. Wakati vifaa maalum vya matibabu vilipopungua, alitumia mbinu mbadala kwa kutumia rasilimali zilizokuwapo. Tiba za kawaida hazikuonyesha mafanikio makubwa, hali iliyomfanya Liu kukumbuka uzoefu wake nchini China wa kutumia marham ya ichthammol kulainisha tishu zilizoambukizwa na kuwa ngumu.
Upasuaji ulipofanyika hatimaye, ilithibitika kuwa mgumu zaidi kuliko ilivyotarajiwa. Maambukizi ya muda mrefu yalikuwa yameifanya tishu kuwa dhaifu sana, zikichanika kwa urahisi hata kwa mvutano mdogo. Upasuaji uliotarajiwa kuchukua dakika 20 uliendelea kwa saa mbili, huku Liu akishona kwa umakini, hatua kwa hatua, gauni lake la upasuaji lililowa jasho.
Uponaji ulimzidi matarajio, na mgonjwa akaruhusiwa kuondoka hospitalini mapema. Wakati Liu alipomwambia kuwa angeweza kuruhusiwa kurudi nyumbani ndani ya wiki moja, Omar alimshika mkono wake kwa nguvu na kusema huku akilia, "Ili kukukumbuka milele, nitampa binti yangu jina la 'Liu.' Kwa njia hiyo, sitakusahau kamwe."
Omar amepona kabisa tangu wakati huo. Baadaye alirudi hospitalini akiwa na mtoto wake kumtembelea daktari huyo Mchina aliyemsaidia kuokoa maisha yake. Mumewe, Mohammed Omar Talib, amesema familia yake inaendelea kuwa na shukurani za dhati.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



