Ubalozi wa Marekani wakata mawasiliano na Spika wa Bunge la Poland kutokana na matusi dhidi ya Trump

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 06, 2026

Picha hii iliyopigwa Januari 1, 2026 ikionyesha mandhari ya Mji Mkongwe wa Warsaw, Poland baada ya theluji kubwa kuanguka. (Picha na Aleksy Witwicki/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Januari 1, 2026 ikionyesha mandhari ya Mji Mkongwe wa Warsaw, Poland baada ya theluji kubwa kuanguka. (Picha na Aleksy Witwicki/Xinhua)

WARSAW - Balozi wa Marekani nchini Poland Tom Rose amesema kuwa Ubalozi wa Marekani nchini humo hautakuwa na mawasiliano yoyote tena na Spika wa Bunge la Poland Wlodzimierz Czarzasty baada ya yeye kumtukana Rais wa Marekani Donald Trump.

Rose amesema uamuzi huo umefuatia "matusi ya kughadhabishana yasiyo na sababu" aliyotoa Czarzasty kwa Trump. "Hatutaruhusu mtu yeyote kuathiri uhusiano kati ya Marekani na Poland, wala kumdharau (Trump)..." ameandika kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii wa X jana Alhamisi.

Siku ya Jumatatu, spika huyo wa Bunge la Poland Czarzasty alisema hataunga mkono pendekezo la kumpa Trump Tuzo ya Amani ya Nobel, akisema hastahili kulipata. 

Picha hii iliyopigwa Machi 20, 2025 ikionyesha mandhari ya Nuuk, Greenland, eneo linalojitawala la Denmark. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

Picha hii iliyopigwa Machi 20, 2025 ikionyesha mandhari ya Nuuk, Greenland, eneo linalojitawala la Denmark. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

Spika huyo alikosoa tishio la Trump la kuichukua Greenland na kutoza ushuru kwa bidhaa za nchi za Ulaya, akisema vitendo hivyo vimekiuka vitendo vya kisiasa vilivyowekwa kwenye kanuni na maadili, na huwa ni vitendo vya kukiuka sheria za kimataifa."

Akijibu balozi huyo wa Marekani Rose, spika Czarzasty ameiambia tovuti ya habari ya Poland, Onet kwamba anashikilia msimamo wake huo juu ya jambo hilo.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha