Kenya kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China

(CRI Online) Februari 06, 2026

Kenya inaendelea na maandalizi kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ijayo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China wakati huu ambapo umaarufu wa filamu za Kichina unaongezeka siku hadi siku katika nchi hiyo.

Taasisi za utamaduni, wadau wa sekta ya utalii na sekta ya ubunifu wanapanga shughuli mfululizo za kukaribisha Mwaka Mpya wa Jadi wa Farasi ambao utaanza Februari 17.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Filamu ya Kenya (KFC) Timothy Owase amesema Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC) limeandaa vipindi vinavyohusu utamaduni wa China, ambavyo wenyeji wana hamu kubwa ya kuvitazama.

Amebainisha kuwa Wakenya wamekuwa wakitazama filamu za Kung Fu za Kichina kwa muda mrefu, lakini kwa sasa wanaonekana kupenda aina nyingine za filamu za China.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha