Lugha Nyingine
Rais wa Kongo Sassou Nguesso atangaza nia ya kugombea muhula ujao
Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso ametangaza nia ya kugombea tena katika uchaguzi wa rais utakaofanyika Machi 15 mwaka huu.
Sassou Nguesso ametoa tangazo hilo jana Alhamisi wakati wa ufunguzi wa maonyesho makubwa ya kwanza ya kilimo nchini humo, ambayo yamepangwa kufanyika hadi Februari 15 katika eneo la Bambou-Mingali la wilaya ya Ignie, umbali wa kilomita 60 kaskazini mwa mji mkuu, Brazzaville.
“Nitaendelea kuunga mkono harakati za kilimo ambazo niliamua kuzizindua mwaka 2021. Kwa hiyo, ninajitangaza mwenyewe, kuwa mgombea kwa uchaguzi wa Machi wa rais,” amesema.
Katika uchaguzi huo, Rais Sassou Nguesso atawania urais akiwa mgombea wa Presidential Majority, muungano wa kisiasa unaojumuisha vyama 18 vya kisiasa. Vyama hivyo vilitia saini tamko la pamoja Februari 2 kuunga mkono ugombea wake.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



