Lugha Nyingine
Somalia yazindua bodi ya ulinzi ili kuimarisha mpito wa usalama
(CRI Online) Februari 03, 2026
Somalia imezindua Bodi mpya ya Ulinzi jana Jumatatu ili kuimarisha usimamizi wa ulinzi, kuongeza uratibu miongoni mwa taasisi za ulinzi, na kuunganisha operesheni na mageuzi ya kijeshi.
Waziri wa Ulinzi wa Somalia Ahmed Moallim Fiqi amesema kuwa bodi hiyo itachukua jukumu kuu katika kuunda mwelekeo wa kimkakati wa ulinzi wa nchi, wakati ambapo serikali inajiandaa kuchukua jukumu kamili la ulinzi wa taifa.
Fiqi pia amesisitiza umuhimu wa kuimarisha uwezo wa vikosi vya jeshi, akibainisha kuwa usalama wa siku zijazo wa Somalia unaweza kuhakikishwa kupitia kujenga kikosi cha kitaaluma chenye uwezo wa kiutendaji na kifedha. Ameongeza kuwa serikali inaendelea kutekeleza mpito uliopangwa ili kuchukua jukumu kamili la usalama wa taifa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



