Reli ya kubeba mizigo mizito ya kwanza ya jangwani barani Afrika iliyojengwa na China yaanza kutoa huduma nchini Algeria

(CRI Online) Februari 03, 2026

Njia ya Reli ya Western Mining ya Algeria, reli ya kubeba mizigo mizito ya kwanza ya jangwani barani Afrika, imeanza kutoa huduma, ikiboresha mtandao wa reli wa Algeria, na kuhimiza muunganisho na maendeleo ya kiuchumi katika maeneo ya kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria ametangaza kuanza rasmi kwa huduma za reli hiyo kwenye hafla iliyofanyika Jumapili katika Jimbo la Bechar, kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Reli hiyo yenye urefu wa kilomita 950, huku kilomita 575 zikijengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Reli ya China (CRCC) na kampuni za kitaifa za Algeria, inawakilisha mradi mkubwa zaidi wa miundombinu uliojengwa na kampuni ya China nchini Algeria.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini humo, reli hiyo itakuwa na uwezo wa kusafirisha tani milioni 50 za madini ya chuma kwa mwaka, pia itakidhi mahitaji ya usafirishaji wa abiria, na kurahisisha maisha ya wakazi wenyeji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha