Lugha Nyingine
Reli zenye urefu wa “Kilomita 50,000” zaonesha Picha ya maendeleo ya mambo ya kisasa
Reli za China sasa zinatoa msukumo wenye nguvu zaidi kwa kuchangia mambo ya kisasa duniani. Siku za karibuni, chombo cha habari cha Marekani kimechambua kwa makini mafanikio ya reli za nchini China kuzidi urefu wa kilomita 50,000, kikisema kuwa mafanikio ya mtandao wa reli za China yameweka mfano wa kuigwa kwa nchi nyingine zinazotafuta njia ya kukamilisha mfumo wao wa reli.
Kupatikana kwa mafanikio hayo ya "kilomita 50,000" kunatokana na kushikilia malengo ya muda mrefu. Kujenga njia za reli kunahitaji kufanya kazi kwa muda mrefu na kutoa uwekezaji mkubwa, hivyo ni lazima kupanga kwanza mpango ndipo kazi zinapoweza kusukumwa mbele kwa njia ya kisayansi. Katika ujenzi wa reli ya mwendokasi, China imewezesha sekta za viwanda na taaluma vishirikiane na visaidiane, ambapo vimeondoa vizuizi vya kiteknolojia, na kuifanya China kuwa nchi inayoongoza badala ya kufuata katika kujenga reli ya mwendo kasi ya kisasa na ya kijani.
Vyombo vya habari vya kimataifa vimechambua "nguvu ya kujikita" ya China katika malengo yao vikisema: Hayo si mafanikio tu, ambayo yanawakilisha njia moja ya kufikiria, "ni matokeo ya nchi kufanya ujenzi kwa kutupia macho karne ijayo badala ya uchaguzi ujao." Kwa kuangalia dunia nzima, wakati baadhi ya nchi zinaposumbuliwa na "siasa ya kukataa" na kukumbwa na tatizo la ujenzi wa miundombinu wa muda mrefu, China imeonesha uthabiti na uendelevu wa sera yake.
Hivi leo, reli za China zinaleta msukumo wenye nguvu zaidi kwa mambo ya kisasa ya dunia. Reli ya Mwendokasi ya Jakarta-Bandung imewasaidia watu wa Indonesia kutimiza "ndoto ya reli ya mwendokasi", na kuhimiza viwanda kando za reli kustawi kwa kasi; Reli ya China-Laos imebadilisha Laos kutoka nchi inayokosa bandari kuwa nchi yenye njia muhimu ya mawasiliano, na kuwatolea watu nafasi za ajira zaidi ya 100,000.
Dunia inaweza kunufaika kwa pamoja na mafanikio ya China. China siyo tu ina uwezo wa kupanga mpango kwa muda mrefu na nguvu ya kutekeleza kila kilichopangwa, bali pia inashikilia siku zote nia ya kufungua mlango na kushirikisha pande nyingi, kunufaishana na kutafuta maendeleo kwa pamoja, na kuleta msukumo wenye nguvu kwa kuchangia kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



