Libya yatoa heshima kwa marehemu Mnadhimu Mkuu wa Jeshi wakati miili ikirejeshwa kutoka Uturuki

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2025

Hafla ya kuaga kijeshi ikifanyika kwa ajili ya miili ya mnadhimu mkuu wa Jeshi la Libya marehemu Mohammed al-Haddad na wenzake, waliopoteza maisha kwenye ajali ya ndege nchini Uturuki mapema wiki hii, mjini Ankara, Uturuki Desemba 27, 2025. (Mustafa Kaya/ kupitia Xinhua)

Hafla ya kuaga kijeshi ikifanyika kwa ajili ya miili ya mnadhimu mkuu wa Jeshi wa Libya marehemu Mohammed al-Haddad na wenzake, waliopoteza maisha kwenye ajali ya ndege nchini Uturuki mapema wiki hii, mjini Ankara, Uturuki Desemba 27, 2025. (Mustafa Kaya/ kupitia Xinhua)

TRIPOLI - Libya ilifanya hafla rasmi Jumamosi kupokea miili ya mnadhimu mkuu wa jeshi marehemu Mohammed al-Haddad na maofisa wenzake, ambao walipoteza maisha kwenye ajali ya ndege nchini Uturuki mapema wiki iliyopita. Miili hiyo ilisafirishwa hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Tripoli, ambapo ilipokelewa na maafisa waandamizi wa Libya akiwemo mkuu wa Baraza la Rais wa Libya Mohamed al-Menfi na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdul-Hamid Dbeibah.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Libya, mkuu huyo wa Baraza la Rais Al-Menfi alimpandisha cheo al-Haddad baada ya kufariki, na kumpa hadhi ya "Field Marshal" kama kutambua utumishi wake.

Shirika hilo la habari limeripoti kuwa, Waziri Mkuu Dbeibah ameahidi kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo, akisema mamlaka za Libya zinashirikiana kwa karibu na Uturuki ili kubaini mazingira yote ya ajali hiyo.

Mapema Jumamosi, hafla ya kuaga kijeshi ilifanyika kwenye Kambi ya Kikosi cha Anga ya Murted mjini Ankara, Uturuki, ikihudhuriwa na maafisa wa ngazi ya juu wa Uturuki wakiwemo Waziri wa Ulinzi Yasar Guler na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Selcuk Bayraktaroglu, ambaye baadaye alisafiri kwenda Libya kwa ajili ya hafla ya kupeleka miili hiyo nyumbani, Shirika la Anadolu la Uturuki liliripoti.

Al-Haddad na maafisa wengine wanne wa kijeshi wa Libya walifariki dunia Jumanne wiki iliyopita wakati walipokuwa wakisafiri kwa ndege ya kibiashara iliyoanguka kusini mwa Ankara. Kabla ya tukio hilo, Al-Haddad alikuwa katika mji mkuu huo wa Uturuki kwa mazungumzo ya kijeshi ya ngazi ya juu.

Libya imeendelea kubaki katika mgawanyiko tangu uasi wa mwaka 2011 uliomwondoa madarakani kiongozi wa zamani Muammar Gaddafi.

Nchi hiyo imegawanyika kati ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa mjini Tripoli, na utawala wa mashariki unaoungwa mkono na Jeshi la Kitaifa la Libya (LNA) chini ya uongozi wa Khalifa Haftar.

Baada ya ajali hiyo, Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, wakati huohuo Jeshi la Kitaifa la Libya lilitoa salamu za rambirambi.

Hafla ya kuaga kijeshi ikifanyika kwa ajili ya miili ya mnadhimu mkuu wa Jeshi la Libya marehemu Mohammed al-Haddad na wenzake, waliofariki dunia kwenye ajali ya ndege nchini Uturuki mapema wiki hii, mjini Ankara, Uturuki Desemba 27, 2025. (Mustafa Kaya/ kupitia Xinhua)

Hafla ya kuaga kijeshi ikifanyika kwa ajili ya miili ya mnadhimu mkuu wa Jeshi la Libya marehemu Mohammed al-Haddad na wenzake, waliofariki dunia kwenye ajali ya ndege nchini Uturuki mapema wiki hii, mjini Ankara, Uturuki Desemba 27, 2025. (Mustafa Kaya/ kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha