AU yakataa utambuzi wa aina yoyote wa Somaliland

(CRI Online) Desemba 29, 2025

Majengo ya makao makuu ya Umoja wa Afrika (Picha/Xinhua)

Majengo ya makao makuu ya Umoja wa Afrika (Picha/Xinhua)

Umoja wa Afrika umesema unakataa utambuzi wa aina yoyote wa Somaliland, kufuatia tangazo la Israel kwamba inaliona eneo hilo lililojitangaza kujitenga la Somalia kuwa ni taifa huru.

Taarifa iliyotolewa Ijumaa iliyopita imesema, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Mahamoud Ali Youssouf amebaini kwa wasiwasi mkubwa hali inayoendelea hivi sasa kuhusu Somaliland.

“Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU anakataa kithabiti mpango au kitendo chochote kinacholenga kuitambua Somaliland kuwa taifa huru, akirudia wito kuwa Somaliland inabaki kuwa sehemu muhimu ya Jamhuri ya Shirikisho la Somalia.” taarifa hiyo inasomeka.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa, jaribio lolote la kupuuza umoja, mamlaka halali, na ukamilifu wa ardhi ya Somalia linakwenda kinyume na kanuni za msingi za Umoja wa Afrika na lina hatari ya kuweka mfano hatari wenye athari kubwa kwa amani na utulivu kote barani Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha