Bandari ya Lianyungang yakaribisha kundi kubwa zaidi la watalii wa Korea Kusini chini ya sera ya China ya msamaha wa visa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2025

Picha ikionyesha meli ya utalii ya "Harmony Yungang" ikiwasili kwenye Bandari ya Lianyungang ya Mji wa Lianyungang, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China, Desemba 28, 2025. (Picha/IC)

Picha ikionyesha meli ya utalii ya "Harmony Yungang" ikiwasili kwenye Bandari ya Lianyungang ya Mji wa Lianyungang, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China, Julai 17, 2025. (Picha/IC)

Jumla ya watalii 255 wa Korea Kusini wamewasili Lianyungang katika Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China jana Jumapili wakiwa wamepanda meli ya utalii ya "Harmony Yungang", na kuanza safari ya utalii ya siku tano ya Mwaka Mpya nchini China. Watalii hao ni wa kundi kubwa zaidi la Korea Kusini kupokelewa kwenye kituo cha abiria cha Bandari ya Lianyungang tangu kuanza kwa sera ya China ya msamaha wa visa kwa raia wa Korea Kusini.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha