Lugha Nyingine
Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao yaharakisha ukuaji wa uchumi wa anga ya chini

Washiriki wa mkutano wakitembelea eneo la maonyesho ya Mkutano wa Maendeleo yenye Sifa Bora ya Uchumi wa Anga Chini wa Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao (GBA), Desemba 25, 2025. (Xinhua/Lu Hanxin)
GUANGZHOU, Desemba 25 – Mkutano wa Maendeleo yenyeSifa Bora ya Uchumi wa Anga Chini wa Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao (GBA) wa mwaka 2025 umefanyika Alhamisi mjini Guangzhou, Kusini mwa China, na kuwaleta pamoja maofisa wa serikali, viongozi wa viwanda, wasomi na wataalamu wengi kujadili mkakati wa ukuaji unaoendeshwa na uvumbuzi katika sekta hiyo.
Mkutano huo umepata matokeo muhimu ya ushirikiano, ambapo miji ya Hong Kong, Macao, Guangzhou na Zhuhai ilisaini mikataba ya inayohusisha ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi, miungano ya taasisi za utafiti, na uvumbuzi wa uendeshaji. Hatua hizi zinalenga kujengamfumo wa mtandao wa viwanda, na kuharakisha ukuaji na mafungamano ya matumizi ya anga ya chini.
Mkoa wa Guangdong unaongoza nchini katika uzalishaji wa droni za matumizi ya kiraia, ikiwa na asilimia 95 ya soko la droni za matumizi ya nyumbani, na asilimia 54 ya soko la droni za matumizi ya viwandani. takwimu hizo ndizo zinazotoa nguvu kwa Guangdong, pamoja na Hong Kong na Macao kushirikiana kusukuma mbele ustawi wa uchumi wa anga ya chini.
Waraka kuhusu Uchumi wa Anga ya Chini wa Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong–Hong Kong–Macao (GBA) Mwaka 2025 uliotolewa na Shirika la Taarifa za Uchumi la China unasisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimsingi kati ya Guangzhou, Shenzhen na Zhuhai kama vituo vya msingi, sambamba na kuimarisha muunganiko wa kina wa Hong Kong na Macao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



