Lugha Nyingine
Watu wanane wafariki baada ya jengo kuporomoka nchini Misri
(CRI Online) Desemba 26, 2025
![]() |
| (Picha/Xinhua) |
Idadi ya watu waliofariki baada ya jengo la ghorofa tano mkoani Giza, Misri, kuporomoka imeongezeka na kufikia nane.
Shirika la Habari Mtandaoni la Ahram linaloendeshwa na serikali ya nchi hiyo limesema, timu za uokoaji zimepata mwili wa mtu mmoja baada ya zoezi la utafutaji na kuondoa kifusi lililodumu kwa siku mbili.
Jengo hilo liliporomoka jumanne wiki hii katika eneo la Imbaba lenye wakazi wengi, na kusababisha majengo ya jirani kuharibika, na watu katika majengo hayo kuhamishwa kama hatua ya tahadhari wakati tathmini ya usalama wa majengo hayo ikifanyika.
(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




