Lugha Nyingine
Rais wa Angola atangaza kuwekeza katika satalaiti mpya

Rais Joao Lourenco wa Angola akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Ufadhili wa Luanda kwa Maendeleo ya Miundombinu ya Afrika mjini Luanda, Angola, Oktoba 28, 2025. (Picha na Julio Kikebu/Xinhua)
LUANDA - Angola itaongeza uwekezaji katika sekta ya mawasiliano ya simu, ambao ni pamoja na mipango ya kurusha satalaiti mpya ya uchunguzi wa Dunia na kupanua mtandao wa mkongo wa taifa wa mawasiliano, ikiwa ni sehemu ya mkakati mpana zaidi wa ujenzi wa mambo ya kisasa na ujumuishaji wa kidijitali wa nchi hiyo.
Rais Joao Lourenco wa Angola ametangaza hilo kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Ufadhili wa Luanda kwa Maendeleo ya Miundombinu ya Afrika uliofanyika mjini Luanda, juzi Jumanne.
Rais Lourenco amesema serikali ya Angola imedhamiria kuhakikisha upatikanaji sawa wa teknolojia za kidijitali na kutumia uvumbuzi wa kiteknolojia kwa maendeleo ya taifa.
"Katika mawasiliano ya simu, tunawekeza katika satalaiti nyingine ya uchunguzi wa Dunia na kupanua mtandao wa mkondo wa taifa wa mawasiliano kote nchini ili kufanya suluhu za kidijitali na uvumbuzi wa kiteknolojia kupatikana kwa Waangola wote," Rais Lourenco amesema.
Angola ilirusha satalaiti yake ya kwanza ya taifa ya mawasiliano ya simu, Angosat-2, mwezi Oktoba 2022. Inatoa huduma kote Angola na sehemu kubwa ya Afrika, ikiboresha upatikanaji wa intaneti, huduma za utangazaji, na mawasiliano ya data.
Serikali ya Angola imesema inawekeza katika miradi muhimu ya teknolojia ya upashanaji habari na mawasiliano, ambayo inachukuliwa kuwa nguzo za kimkakati za kuufanya uchumi wake kuwa wenye kutegemea sekta mbalimbali na ya mafungamano ya kikanda, katika kuendana na Ajenda ya Umoja wa Afrika ya 2063.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



