Lugha Nyingine
Tanzania yaweka marufuku ya kutembea usiku kufuatia maandamano makubwa yaliyotokea siku ya uchaguzi
Jeshi la Polisi nchini Tanzania jana Alhamisi jioni lilitangaza marufuku ya kutoka nje katika mji wa Dar es Salaam kufuatia maandamano ya siku nzima hiyo yaliyosababisha uharibifu wa mali katika siku ya uchaguzi mkuu nchini humo.
"Baada ya saa 12 jioni (kwa saa za Tanzania) hakuna mtu ataruhusiwa kuonekana katika mitaa ya Dar es Salaam isipokuwa polisi ambao watakuwa kwenye kazi maalum" Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi la Tanzania Camillus Wambura amesema kupitia televisheni.
Hata hivyo, hakufafanua ni kwa muda gani marufuku hiyo itadumu.
Pia, upatikanaji wa intaneti nchini humo umeripotiwa kutatizwa.
Kumekuwa na ripoti kwamba waandamanaji walikuwa wakikabiliana kwa vurugu na polisi, ambao walijibu kwa kufyatua risasi. Aidha, baadhi ya vituo vya polisi, vituo vya mafuta, mabasi na vituo vya kura vimeripotiwa kuharibiwa na waandamanaji hao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



