Angola yawa mwenyeji wa mkutano wa muunganiko wa nishati na uwekezaji wa kijani

(CRI Online) Oktoba 30, 2025

Mkutano wenye kaulimbiu "Muunganiko wa Nishati na Uwekezaji wa Kijani: Kuboresha Mustakabali wa Pamoja wa Kijani barani Afrika” umefanyika katika mji mkuu wa Angola, Luanda, Jumanne wiki hii.

Mkutano huo uliandaliwa kwa pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Umoja wa Afrika, Ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika, na Shirikisho la Maendeleo na Ushirikiano wa Nishati Duniani, ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Ufadhili wa Luanda kwa Maendeleo ya Miundombinu barani Afrika.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Teknolojia, Uvumbuzi, Muunganiko na Miundombinu katika Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Afrika, Robert Lisinge amesema, Afrika inaendelea kukabiliwa na changamoto katika upatikanaji wa nishati na muunganiko wa miundombinu, huku ikikabiliwa na pengo kubwa la uwekezaji.

Amesema muunganiko wa nishati kikanda na uwekezaji wa nishati ya kijani ni vichocheo muhimu kwa maendeleo endelevu na uhimilivu wa mabadiliko ya tabianchi, akirejea dhamira ya Kamisheni hiyo ya kuimarisha ushirikiano na wadau wote husika.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha