UNGA yapitisha mswada wa azimio linaloihimiza Marekani kumalizia vikwazo dhidi ya Cuba

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 30, 2025

Watu wakitembea kuupita mchoro na maandishi ya ukutani yanayolaani vizuizi vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya Cuba, mjini Havana, mji mkuu wa Cuba, Septemba 22, 2025. (Picha na Joaquin Hernandez/Xinhua)

Watu wakitembea kuupita mchoro na maandishi ya ukutani yanayolaani vizuizi vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya Cuba, mjini Havana, mji mkuu wa Cuba, Septemba 22, 2025. (Picha na Joaquin Hernandez/Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) limepitisha mswada wa azimio jana Jumatano likiihimiza Marekani kumalizia vikwazo vyake vya kiuchumi, kibiashara na kifedha dhidi ya Cuba.

Mswada huo umepitishwa kwa kura 165 za ndio, saba za hapana na 12 za kujizuia. Argentina, Hungary, Israeli, Macedonia Kaskazini, Paraguay, Ukraine na Marekani zimepiga kura kupinga azimio hilo.

Mswada huo umesisitiza tena wito wa UNGA kwa nchi wanachama wote wa Umoja wa Mataifa kujiepusha kutangaza na kutumia sheria na hatua za aina iliyorejelewa katika utangulizi wa maandishi ya mswada huo, kwa kutii wajibu wao chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa na sheria ya kimataifa, ambayo pamoja na mambo mengine, inathibitisha tena uhuru wa biashara na usafirishaji wa meli.

Pia linahimiza nchi wanachama "ambazo zimetumia na zinaendelea kutumia sheria na hatua za namna hiyo kuchukua hatua muhimu za kuzifuta au kuzibatilisha haraka iwezekanavyo kwa mujibu wa utaratibu wao wa sheria."

Tangu mwaka 1992, UNGA imekuwa ikipitisha kwa kura nyingi azimio la mwaka lisilolazimisha kisheria, likiihimiza Marekani kumalizia vikwazo vyake dhidi ya Cuba vilivyowekwa tangu mwaka 1962.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha