Jukwaa la 2025 juu ya Maendeleo ya Xizang, China lafuatilia mageuzi ya Xizang na maendeleo ya siku za baadaye

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 30, 2025

Picha hii iliyopigwa Oktoba 29, 2025 ikionyesha hafla ya ufunguzi wa "Jukwaa la 2025 juu ya Maendeleo ya Xizang, China" katika Mji wa Nyingchi, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China. (Xinhua/Jiang Fan)

LHASA – Maafisa wa serikali, wanadiplomasia, wataalamu kutoka sekta mbalimbali, na wawakilishi wa kampuni za kiviwanda na vyombo vya habari zaidi ya 400 kutoka nchi na maeneo 44 walikusanyika jana Jumatano katika Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China kuhudhuria Jukwaa la 2025 juu ya Maendeleo ya Xizang, China ili kuchangia maarifa na utaalamu wao kwa ajili ya maendeleo endelevu ya mkoa huo.

Jukwaa hilo, linaloandaliwa na serikali ya mkoa huo wa Xizang na likibeba mada kuhusu kaulimbiu ya "Kugundua Xizang inayopendeza na kuandika ukurasa mpya kwenye uwanda," limefuatilia katika mada muhimu zikiwemo za mawasiliano ya kimataifa, miongozo ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ya kuiongoza Xizang katika zama mpya, na ujengaji taswira ya Xizang, falsafa zake za maendeleo na njia za kivitendo.

Jukwaa hilo la mwaka huu linafanyika wakati Xizang inapoadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwake.

"Katika kipindi cha miaka 60 iliyopita, chini ya uongozi wa CPC, Xizang imepata maendeleo makubwa ya kihistoria kutoka kuwa nyuma kimaendeleo hadi kupiga hatua kimaendeleo, kutoka kutengwa hadi kufungua mlango, na kutoka umaskini hadi ustawi," Wang Junzheng, Katibu wa Kamati ya CPC ya Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, amesema katika hotuba yake.

Ameongeza kuwa, Xizang imefanikisha katika miongo michache tu kile ambacho kingechukua karne au hata milenia, ikitumika kama ushuhuda dhahiri wa nguvu za mfumo wa ujamaa.

Akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi, Mo Gaoyi, naibu mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China, amesisitiza kwamba wakati ambapo China inaandaa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano ya maendeleo ya uchumi na kijamii ya taifa, ujenzi wa mambo ya kisasa wa Xizang sasa uko katika hatua mpya ya kihistoria.

"Tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 2007, jukwaa hili limekuwa dirisha muhimu kwa jumuiya ya kimataifa kuelewa, kuchunguza na kupata ufahamu kuhusu Xizang," Mo amesema.

Wasanii wakiimba na kucheza ngoma kwenye hafla ya ufunguzi wa "Jukwaa la 2025 juu ya Maendeleo ya Xizang, China" katika Mji wa Nyingchi, Mkoani Xizang, kusini magharibi mwa China, Oktoba 29, 2025. (Xinhua/Jiang Fan)

Jukwaa hilo la siku moja limefanyika katika Mji wa Nyingchi, mahali ambapo hapo awali palikuwa pembezoni mbali na palipotengwa, pakijulikana katika nyakati za kale kama mahali pa uhamishoni. Leo, mji huo unashindana na Lhasa kwa umaarufu na umekuwa moja ya maeneo maarufu zaidi ya utalii nchini China.

Shahbaz Khan, mkurugenzi na mwakilishi wa Ofisi ya Kikanda ya UNESCO kwa Asia Mashariki, akitoa hotuba kwenye hafla ya ufunguzi wa "Jukwaa la 2025 juu ya Maendeleo ya Xizang, China" katika Mji wa Nyingchi, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Oktoba 29, 2025. (Xinhua/Jiang Fan)

"Simulizi ya Xizang ni moja ya mageuzi," Shahbaz Khan, mkurugenzi na mwakilishi wa Ofisi ya Kikanda ya UNESCO kwa Asia Mashariki, amesema katika hotuba yake ya ufunguzi iliyotolewa kwa niaba ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, akiongeza kuwa: "Tunashuhudia eneo ambalo hapo awali lilikuwa pembezoni mbali sasa linasimama likiwa limeunganishwa kupitia miundombinu ya kisasa inayounganisha hata mabonde yake ya juu zaidi na jamii zilizo mbali zaidi."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha