Lugha Nyingine
Kwa nini kampuni za kigeni zinaongeza uwekezaji wa utafiti na maendeleo nchini China?
Tokea mwaka huu, uwekezaji wa kampuni za kigeni nchini China umeonekana kuwa na mwelekeo dhahiri: Kampuni kubwa za kimataifa zinazidisha uwekezaji wa utafiti na maendeleo nchini China na kuharakisha kuanzisha vituo vya utafiti na maendeleo. Kutokana na takwimu zilizotolewa na Taasisi ya Utafiti ya Wizara ya Biashara, hadi mwezi wa Septemba mwaka huu, idadi ya vituo vya utafiti na maendeleo vya kampuni za kigeni mjini Shanghai imefikia 631. Na hadi mwezi wa Januari mwaka huu, idadi ya vituo vya aina hiyo mjini Beijing imefikia 221.
Hivi karibuni, Kampuni ya Bosch ya Ujerumani imesaini makubaliano na Eneo la Viwanda la Suzhou ambayo yalipanga kufanya uwekezaji takribani yuan bilioni 10 katika miaka mitano ijayo kwa kujenga mradi wa viwanda vya uvumbuzi wa uendeshaji na udhibiti wa magari kwa teknolojia ya AI, unalenga kufanya utafiti na maendeleo ya mfumo wa kisasa wa jumuishi wa uendeshaji wa magari kwa teknolojia ya AI, na kuzalisha bidhaa zinazohusika za programu na zana na vifaa vya viti vya gari kwa teknolojia ya AI. Katika mji wa Jiaxing, Mkoani Zhejiang, kampuni ya Danfoss Group ya Denmaki, imeongeza uwekezaji wa yuan bilioni 2.7, ikiwa ni mara yake ya kumi ya kuongeza uwekezaji katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita.
Katika sekta nyingi za teknolojia za kisasa, China imekuwa nchi ya kuongoza soko. “Kutafiti na kujiendeleza nchini China ili kutoa huduma kwa dunia nzima” yamekuwa mahitaji ya ndani kwa kampuni nyingi kubwa za kimataifa kwa ajili ya kudumisha na kuongeza nguvu zao za ushindani katika soko. Uwekezaji wa China katika utafiti na maendeleo unazidi wastani wa kiwango cha nchi za Umoja wa Ulaya. China ilichukua nafasi ya kumi katika kazi za uvumbuzi duniani. Makundi 24 ya uvumbuzi ya China ambayo yanashirikisha viwanda, taasisi na vyuo vikuu, yaliorodheshwa kwenye makundi 100 bora duniani. Serikali, kampuni na watumiaji wote wanaunga mkono na kupokea mambo ya uvumbuzi, hali hii imeanzisha hali ya mzunguko mzuri kati ya teknolojia na soko.
Mvuto wa China umehusiana moja kwa moja na ufunguaji mlango. Kutokana na kuboreshwa siku hadi siku mazingira ya biashara, kutoka kampuni za kigeni kupata huduma sawasawa na kampuni za China katika manunuzi ya serikali, hadi kuimarisha haki miliki ya ubunifu wa nje katika mfumo wa uvumbuzi, yote hayo yamehimiza mashirikiano baina ya uwekezaji wa kigeni na upanuzi wa ufunguaji mlango wa China.
Mkutano wa Nne wa Wajumbe Wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ulisema: “Kuendeleza ufunguaji mlango kwa kuhimiza mageuzi na maendeleo, kunufaika pamoja na fursa ili kupata maendeleo kwa pamoja na nchi nyingine.” Umuhimu wa China katika uchumi wa dunia unazidi kuongezeka, lakini nia ya awali ya China haitabadilika: China inapenda kunufaika fursa ya maendeleo pamoja na nchi nyingine ili kushirikiana na nchi mbalimbali katika kuanzisha siku nzuri za baadaye zenye mustakabali bora zaidi wa maendeleo na za jumuishi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



