Lugha Nyingine
China kushirikiana na pande zote Kuunga Mkono Mfumo wa Kimataifa wa Kuondoa na Kutoeneza Silaha za Nyuklia
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 29, 2025
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Guo Jiakun amesema, ikiwa ni nchi mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja Mataifa na taifa lenye silaha za nyuklia linalowajibika, China imekuwa ikifuata njia ya maendeleo ya amani, na itafanya kazi na pande zote ili kuunga mkono mamlaka ya Mkataba wa Kupiga Marufuku kwa pande zote Majaribio ya Nyuklia (CTBT), na kulinda mfumo wa kimataifa wa kuondoa na kutoeneza silaha za nyuklia.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumanne, Bw. Guo pia amesema, ikiwa moja ya nchi zilizosaini mkataba huo, China imekuwa ikishiriki kikamilifu katika kazi ya Tume ya Maandalizi ya Mkataba huo na kuendelea na maandalizi ya utekelezaji wa mkataba huo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



