Kushikilia ushirikiano wa kunufaishana, na kufanya mashauriano kwa usawa ili kutatua masuala ya uchumi na biashara

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 17, 2025

Pande mbili za China na Marekani zilifanya mazungumzo jijini Madrid, Hispania kuanzia Septemba 14 hadi 15 kwa saa za huko. Kwa kufuata maoni muhimu ya pamoja yaliyofikiwa katika mazungumzo kati ya marais wa nchi hizo mbili kwa njia ya simu, pande hizo mbili zilijadili masuala ya uchumi na biashara yanayofuatiliwa nao pamoja, na kufikia kimsingi maoni ya pamoja kuhusu kushughulikia kwa mwafaka masuala husika ya TikTok kwa njia ya ushirikiano, kupunguza vizuizi vya uwekezaji na kuhimiza ushirikiano husika wa kiuchumi na kibiashara.

Ushirikiano wa kunufaishana ndiyo hali asili ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, na pia ndio msingi wa mazungumzo endelevu kati ya pande hizo mbili. Katika mazungumzo hayo, pande zote mbili zilikubaliana kuwa uhusiano tulivu wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani una umuhimu mkubwa kwa nchi hizo mbili na pia una ushawishi mkubwa kwa utulivu na maendeleo ya uchumi wa dunia. Maoni hayo ya kauli moja yameweka msingi wa kufanya mashauriano zaidi na kutoa dira ya kushughulikia kwa usahihi masuala yanayofuatiliwa nao, na vilevile kuleta imani kwa maendeleo ya uchumi wa dunia.

Suala la TikTok lilikuwa moja ya mada muhimu katika mazungumzo hayo, na kushughulikia masuala husika kwa njia ya kufanya ushirikiano ni maendeleo ya hali ya mambo yaliyopatikana kwa juhudi katika mazungumzo hayo. Upande wa China siku zote unapinga kuyafanya mambo ya teknolojia, uchumi na biashara yawe ya kisiasa, au kuwa vyombo na silaha, na kamwe haitaweza kufikia makubaliano kwa kupoteza kanuni, maslahi ya kampuni au usawa na haki za kimataifa.

Katika mazungumzo hayo, pande mbili China na Marekani zikiwa kwenye msingi wa kuheshimu vya kutosha nia ya makampuni na kanuni za soko, zimefikia maoni ya pamoja ya kimsingi ya kushughulikia suala la TikTok kwa kupitia njia ya kukabidhi upande wa Marekani haki ya matumizi ya hakimiliki ya ubunifu kuhusu uendeshaji na mahesabu (algorithm) ya takwimu za idadi ya watumiaji wa TikTok wa Marekani, na kazi ya usalama wa maudhui.

Sababu ya upande wa China kufikia maoni ya pamoja na Marekani kuhusu TikTok ni kwa kuwa maoni hayo yanafuata kanuni za kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja, na yanaendana na maslahi ya pande zote mbili. Msimamo wa kikanuni wa China wa kulinda kithabiti maslahi ya nchi na haki na maslahi halali za kampuni za China haujabadilika, na China itathibitisha kwa mujibu wa sheria mambo ya TikTok yanayohusika na kazi za kuuza nje teknolojia na kutoa haki ya matumizi ya ubunifu.

Ni lazima kueleza kuwa, baada ya mashauriano mfululizo kuhusu uchumi na biashara, upande wa Marekani bado haujasitisha vitendo vyake vya makosa vya kuchukua hatua za vizuizi vya kiuchumi na kibiashara dhidi ya upande wa China. Upande wa Marekani umekuwa ukipanua kupita kiasi usalama wa nchi, na kuendelea kuongeza idadi ya kampuni za China katika orodha ya kuwekewa vikwazo. Kitendo hicho cha umwamba wa upande mmoja kinakiuka sheria za kimataifa na msingi wa uhusiano wa kimataifa. China imeeleza kwa makini ufuatiliaji wake kwa Marekani kuhusu suala hili katika mazungumzo hayo.

Kufanya mazungumzo kwa usawa na kutafuta ushirikiano wa kunufaishana ni njia bora ya kupunguza migongano na kutatua matatizo. Pande mbili China na Marekani zinapaswa kuendelea kutekeleza maoni muhimu ya pamoja yaliyofikiwa katika mazungumzo ya viongozi wa nchi hizo mbili kwa njia ya simu na matokeo yaliyopatikana katika mazungumzo ya uchumi na biashara yaliyopita, kutumia ipasavyo utaratibu wa mashauriano ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha