

Lugha Nyingine
IGAD yatahadharisha kuwa watu milioni 42 Afrika Mashariki na katika pembe ya Afrika wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula
(CRI Online) Septemba 17, 2025
Jumuiya ya kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD imesema takriban watu milioni 42 wa eneo la Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika wanakabiliwa na viwango vya juu vya ukosefu wa usalama wa chakula kwa mwaka huu.
Ripoti iliyotolewa Jumanne na Jumuiya hiyo imezitaja Djibouti, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Uganda kuwa ni nchi zenye hatari ya kukumbwa na ukosefu wa chakula.
Katika taarifa hiyo IGAD imesema viwango vya njaa katika nchi hizi sita bado viko juu sana. Tano kati ya nchi hizo (Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, na Uganda) idadi ya watu walio kwenye msukosuko mkubwa wa chakula iliongezeka karibu mara tatu, kutoka milioni 13.9 wa mwaka 2016 hadi milioni 41.7 wa mwaka huu.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma