

Lugha Nyingine
Mwakilishi wa China alaani shambulizi la Israeli dhidi ya Qatar
(CRI Online) Septemba 17, 2025
Mkutano wa 60 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lilifanya mjadala wa dharura kuhusu shambulizi la Israeli dhidi ya Qatar kutokana na ombi la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).
Katika mkutano huo, mwakilishi wa China katika ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Balozi Chen Xu amesema, shambulizi la Israeli dhidi ya Qatar ni uvunjaji wa wazi wa mamlaka ya ardhi na usalama wa kitaifa wa Qatar, limekiuka sheria za kimataifa na katiba ya Umoja wa Mataifa, na kuharibu juhudi za amani.
Balozi Chen amesisitiza kuwa, matumizi mabaya ya nguvu si ufumbuzi wa matatizo, na China inapenda kushirikiana na jamii ya kimataifa, kufanya juhudi za kiujenzi katika kusimamisha mapambano, na kupunguza hali ya wasiwasi kwenye eneo hilo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma