Serikali ya DRC na waasi wa M23 kufanya duru mpya ya mazungumzo mjini Doha

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2025

Benjamin Mbonimpa (kulia), Katibu Mkuu wa Muungano wa Mto Kongo (AFC) na mkuu wa ujumbe wake kwenye mazungumzo ya Doha, akihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Julai 3, 2025. (Picha na Zanem Nety Zaidi/Xinhua)

GOMA, DRC - Duru mpya ya mazungumzo kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kundi la waasi la M23 inatarajiwa kufanyika hivi karibuni mjini Doha, mji mkuu wa Qatar, afisa mwandamizi wa Muungano wa Mto Kongo (AFC), muungano wa kisiasa na kijeshi unaoshirikiana na M23, amesema jana Alhamisi.

"Kwa mara ya tano, tutarejea Doha kuendelea na mazungumzo na upande wa serikali chini ya upatanishi wa Qatar," amesema Freddy Kaniki, naibu mratibu wa AFC, kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini, bila kuweka wazi tarehe ya mazungumzo hayo yajayo.

Tangu mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu, duru nne za mazungumzo zimeshafanyika kati ya AFC/M23 na serikali ya DRC, huku Qatar ikiwa kama mpatanishi, kwa mujibu wa Kaniki.

Mwishoni mwa mwezi Aprili, Kinshasa ilitangaza dhamira ya pamoja na M23 katika kusimamisha mapigano na mchakato wa amani.

Benjamin Mbonimpa, katibu mkuu wa AFC na mkuu wa ujumbe wake kwenye mazungumzo hayo ya Doha, ameeleza kwamba "mafanikio fulani" yamepatikana kufuatia mkutano wa mwezi Juni mjini Goma na Bintou Keita, mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kuleta Utulivu nchini DRC.

Juni 27, DRC na Rwanda zilitia saini makubaliano ya amani ya kihistoria nchini Marekani, ikiibua matumaini ya kumaliza vita vya miaka mingi na janga la kibinadamu mashariki mwa DRC na eneo pana la Maziwa Makuu.

Hata hivyo, uwepo wa waasi wa M23 katika sehemu za mashariki mwa DRC bado unabaki kuwa uhalisia katika maeneo mbalimbali na haujashughulikiwa kidhahiri katika makubaliano hayo. Makubaliano hayo yanatambua jukumu la Qatar, ambayo imewezesha duru kadhaa za mazungumzo kati ya Kinshasa na M23.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, watu zaidi ya milioni 27.8 nchini DRC wanakabiliwa na hali ya ukosefu wa usalama wa chakula, huku zaidi ya milioni 7 wakiwa wakimbizi wa ndani, wengi wao mara kadhaa.

Maafisa wa Muungano wa Mto Kongo (AFC) wakihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Julai 3, 2025. (Picha na Zanem Nety Zaidi/Xinhua)

Benjamin Mbonimpa (kulia, mbele), Katibu Mkuu wa Muungano wa Mto Kongo (AFC) na mkuu wa ujumbe wake kwenye mazungumzo ya Doha, akihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Julai 3, 2025. (Picha na Zanem Nety Zaidi/Xinhua)

Benjamin Mbonimpa (wa pili, kulia), Katibu Mkuu wa Muungano wa Mto Kongo (AFC) na mkuu wa ujumbe wake kwenye mazungumzo ya Doha, akihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Julai 3, 2025. (Picha na Zanem Nety Zaidi/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha