Bunge la Marekani lapitisha ‘Muswada Mmoja Mkubwa Mzuri’ wa Trump

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2025

Picha iliyopigwa Julai 3, 2025 ikionyesha jengo la Bunge la Marekani, Capitol mjini Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Hu Yousong)

Picha iliyopigwa Julai 3, 2025 ikionyesha jengo la Bunge la Marekani, Capitol mjini Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Hu Yousong)

NEW YORK - Baraza la Wawakilishi la Marekani limepitisha 'Mswada Mmoja Mkubwa Mzuri' uliotolewa na Rais Donald Trump kwa kura 218 za ndiyo na 214 za hapana jana Alhamisi ambapo mswada huo sasa utatumwa kwa dawati la rais kwa ajili ya kutiwa saini ifikapo tarehe ya mwisho ya Julai 4, ambayo ilikuwa imewekwa na Rais Trump.

Wawakilishi wawili wa chama cha Republican, Thomas Massie wa Kentucky na Brian Fitzpatrick wa Pennsylvania, wamepiga kura dhidi ya mswada huo.

Baraza la Wawakilishi lilipitisha mswada wa awali ya sheria hiyo mwezi Mei na kuituma kwa Seneti, lakini mswada huo ulirekebishwa kwa upana na kupitishwa kwa kura chache na maseneta huku Makamu Rais JD Vance akipiga kura ya kuvunja kizuizi siku ya Jumanne.

Mswada huo kuhusu kodi na matumizi unajumuisha kupunguzwa kwa ushuru na kuongeza fedha za matumizi ya kijeshi na usalama wa mpakani. Kinacholeta mvutano ni kwamba mswada huo unatabiriwa kuongeza dola za kimarekani trilioni 3.3 kwenye deni la taifa kwa sasa likiwa katika kiwango cha juu huku ukiondoa mamilioni ya watu kwenye Huduma za Matibabu na kuponi za chakula.

Haya ni mafanikio makubwa ya kwanza ya Trump katika utungaji sheria katika muhula wake wa pili.

Wabunge wa Chama cha Republican kwenye Baraza la Wawakilishi, Congress walikuwa wamekuwa na maoni ya tofauti kwa kiasi kikubwa kuhusu mswada huo, ambao ulipita kwenye upigaji kura wa Seneti na Baraza hilo la Wawakilishi baada ya rais na washirika wake wa Capitol Hill kuwashinikiza Wabunge hao wa Republican wenye maoni tofauti kusimama kwenye mstari.

Wakati wa kutia saini mswada huo ambao utatumwa kwa rais, Spika wa Bunge Mike Johnson amesema kwamba mswada huo ukipitishwa, "tutalazimika kurekebisha kila eneo la sera ya umma."

"Kila kitu kilikuwa janga kabisa chini ya serikali ya Biden-Harris, yenye msimamo mkali, ulioamka, na wenye uendelevu wa Chama cha Democrat, na tulichukua juhudi bora zaidi tuwezavyo, katika mswada mmoja mkubwa na mzuri, kurekebisha mambo yake mengi tuwezavyo," ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha