

Lugha Nyingine
Iran yasema bado inahitaji muda zaidi kuamua juu ya kuanza tena mazungumzo na Marekani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi akifanya mkutano na waandishi wa habari mjini Istanbul, Uturuki, Juni 22, 2025. (Xinhua/Liu Lei)
TEHRAN - Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi katika mahojiano na Kituo cha Habari cha CBS mjini Tehran, yaliyochapishwa Jumatatu, amesema nchi hiyo bado inahitaji muda zaidi wa kuamua kuhusu kuanza tena mazungumzo na Marekani.
Araghchi ameyasema hayo alipokuwa akitoa maoni yake kuhusu uwezekano wa kuanza tena mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na Marekani.
Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba mazungumzo hayo yanaweza kuanza mapema wiki hii. Araghchi amesema hafikirii mchakato huo unaweza kuanza tena haraka kama Trump alivyosema.
"Ili tuweze kuamua kushiriki tena, itabidi kwanza tuhakikishe kwamba Marekani haitarejea tena kutulenga katika mashambulizi ya kijeshi wakati wa mazungumzo" amesema.
"Na nadhani kwa kuzingatia haya yote, bado tunahitaji muda zaidi," amesema, akibainisha kuwa, hata hivyo, "milango ya diplomasia haitafungwa kamwe."
Juni 22, vikosi vya Marekani vilishambulia kwa mabomu vituo vitatu vya nyuklia vya Irani vya Natanz, Fordow na Isfahan. Katika kulipiza kisasi, Iran ilishambulia kambi ya kikosi cha anga cha Marekani ya Al Udeid nchini Qatar.
Shambulizi hilo lilitokea wakati kukiwa na mgogoro kati ya Iran na Israel, ambao ulianza Juni 13, kwa Israel kufanya mashambulizi ya anga katika miji kadhaa ya Iran. Usimamishaji vita ulitangazwa kati ya pande hizo mbili Juni 24.
Mashambulizi hayo ya Israel yalianzishwa siku chache kabla ya duru ya sita ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na kuondolewa kwa vikwazo vya Marekani, ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika katika mji mkuu wa Oman, Muscat, Juni 15.
Kituo cha mafunzo cha Bajiquan mkoani Hebei, China chakaribisha wanafunzi kutoka Russia
Picha: Mandhari ya mbuga katika majira ya joto mkoani Gansu, China
Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma