Mkuu wa masuala ya kibinadamu wa UN akutana na viongozi wa M23 nchini DRC

(CRI Online) Juni 27, 2025

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu Tom Fletcher amekutana na viongozi wa kundi la M23 mjini Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kuhusu hali ya kibinadamu na mfumo wa ulinzi.

Mkutano huo umefanyika jana alhamis wakati wa ziara ya siku mbili ya Fletcher mashariki mwa DRC, ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika eneo hilo tangu kundi la M23 kukalia mji wa Goma na maeneo ya jirani.

Fletcher amesema ameenda kwenye eneo hilo kusikiliza maoni ya watu wa huko, na kwa pamoja na mamlaka za jeshi za mji wa Goma, kushughulikia suala la dharura la ulinzi wa raia, hasa makundi yaliyo hatarini yanayoathiriwa na mgogoro wa kibinadamu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha