Jukwaa la kwanza la Afrika Magharibi lafanyika Senegal

(CRI Online) April 25, 2025

Jukwaa la kwanza la Afrika Magharibi limefanyika jana Alhamisi mjini Dakar, Senegal, likiwa na kauli mbiu ya "Kuimarisha ushirikiano wa majopo ya washauri bingwa kati ya China na Afrika, na Kuhimiza utandawazi wa kisasa wa China na Afrika."

Jukwaa hilo lilihudhuriwa na wataalamu mashuhuri, wanazuoni, maafisa wa serikali, mabalozi, na waandishi wa habari kutoka China na Afrika.

Kabla ya ufunguzi wa jukwaa hilo, wawakilishi kutoka Taasisi ya Utafiti ya China na Afrika (CASS) na Taasisi ya Taifa ya Utawala ya Senegal (ENA) walisaini taarifa ya pamoja kuhusu kuanzishwa kwa pamoja kwa Kituo cha Utafiti cha China na Afrika.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa Jukwaa hilo, mkuu wa Akademia ya Sayansi ya Jamii ya China (CASS), Gao Xiang, amesema, kusainiwa kwa taarifa hiyo ya pamoja kuna umuhimu mkubwa katika kuimarisha mawasiliano ya kitaaluma, mazungumzo kati ya majopo ya washauri bingwa, na kuhimiza malewano kati ya watu wa nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha