UNECA yasema ushuru wa Marekani unaleta athati mbaya kwa nchi za Afrika

(CRI Online) April 25, 2025

Aliyekuwa katibu mkuu wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika (UNECA) Carlos Lopes amesema, ushuru mpya uliowekwa na Marekani unaleta athari mbaya kwa nchi za Afrika ambazo zimefanya kazi kubwa kuingia katika mnyororo wa thamani wa kimataifa chini ya mfumo wa biashara wa pande nyingi.

Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua, Lopes amesema nchi kama Madagascar, Lesotho na Kenya zimejikuta katika mazingira magumu kwa kuwa zimeendeleza sekta za biashara ya nje kama vitambaa, nguo, na bidhaa za kilimo, ambazo zote zimewekewa nyongeza ya ushuru.

Ameongeza kuwa, Afrika, ambayo imekuwa na unyumbulifu katika kujenga washirika wa kibishara, itaendelea kubadili mtazamo wake kuelekea nchi za Bara la Asia, hususan China na India, nchi za Ghuba na nchi nyingine, ambapo uhusiano mara nyingi unakuwa wa kimkakati, na kivitendo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha