

Lugha Nyingine
Wawakilishi wa China, Russia na Iran wakutana na mkurugenzi mkuu wa IAEA kujadili suala la nyuklia la Iran
(Picha inatoka tovuti ya CRI)
Mwakilishi wa kudumu wa China katika Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia (IAEA) Bw. Li Song, na wenzake wa Russia Bw. Mikhail Ulyanov na wa Iran Reza Najafi wamekutana na mkurugenzi mkuu wa IAEA Bw. Rafael Grossi, wakijadili jinsi IAEA itakavyofanya kazi katika hali ya sasa ili kuhimiza suluhisho la kisiasa na kidiplomasia kwa suala la nyuklia la Iran.
Wawakilishi wa nchi hizo tatu kwenye mazungumzo hayo ya jana Alhamisi wamesisitiza kuwa mawasiliano na mazungumzo ya kidiplomasia yanayofanyika katika msingi wa kuheshimiana ndiyo njia pekee mwafaka kutatua suala hilo na kwamba China na Russia zinaunga mkono Iran kuimarisha ushirikiano na IAEA.
Bw. Li Song ameeleza kuwa China inapongeza ahadi ya Iran ya kutotengeneza silaha za nyuklia na inaheshimu haki ya Iran kutumia nishati ya nyuklia kwa njia ya amani.
Amesema China inaiunga mkono Iran kufanya mazungumzo na pande mbalimbali ikiwemo Marekani, na kulinda maslahi halali kupitia mazungumzo.
“Kutokana na hali mpya ya sasa, China inapenda kuimarisha zaidi ushirikiano na mawasiliano na Russia, Iran na IAEA ili kuingiza nguvu chanya katika mchakato wa kusuluhisha suala la nyuklia la Iran kwa njia ya kidiplomasia” amesema Li.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma