

Lugha Nyingine
Wizara ya Biashara ya China yasema: Hakuna majadiliano yaliyofanywa kati ya China na Marekani kuhusu uchumi na biashara
BEIJING – Hakujafanyika majadiliano yoyote kati ya China na Marekani kuhusu uchumi na biashara, msemaji wa wizara ya biashara ya China He Yadong amesema jana Alhamisi, akiongeza kuwa habari yoyote kuhusu upigaji hatua katika mazungumzo kati ya nchi hizo mbili kuhusu uchumi na biashara hazina msingi hata kidogo, na ni uzushi mtupu tu.
Msemaji He amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akijibu swali husika.
Amesema msimamo wa China ni wa siku zote bila kubadilika, ambao unashikilia msimamo wa uwazi juu ya mashauriano na mazungumzo, lakini mashauriano na majadiliano ya aina yoyote lazima yafanywe katika hali ya usawa kwenye msingi wa kuheshimiana.
"Sisi Wachina si waleta matatizo, lakini hatutakurupuka matatizo yanapotujia. Kuogopesha, vitisho na ulaghai si njia sahihi ya kufanya mawasiliano na China," He amesema.
Msemaji He amesema, "Vita vya kibiashara vimeanzishwa na upande mmoja wa Marekani kwa makusudi," China inaitaka Marekani kusahihisha vitendo vyake vya makosa, ionyeshe udhati kama kweli inataka kufanya mazungumzo, na kurejea kwenye njia sahihi ya kufanya mazungumzo na mashauriano kwa usawa ili kwa pamoja kuhimiza maendeleo tulivu, mazuri, na ya endelevu ya ushirikiano kati ya China na Marekani katika sekta za uchumi na biashara.
"Utozaji kodi ya juu kiholela wa Marekani unakiuka kanuni za kimsingi za uchumi na soko, na si kama tu hautasaidia kutatua matatizo ya ndani ya Marekani bali pia umeharibu vibaya utaratibu wa kimataifa wa uchumi na biashara, na kuvuruga uzalishaji na uendeshaji wa kawaida wa viwanda na matumizi ya kila siku ya watu," He amesema.
Amesema kuwa vitendo hivyo vya Marekani vimepingwa vikali na jumuiya ya kimataifa na ndani ya Marekani yenyewe, na "mfanyaji wa hayo lazima atengue fundo yenyewe".
Amesema hatua hizo za upande mmoja za kuongeza kodi zilianzishwa na Marekani, na kama upande wa Marekani unataka kweli kutatua suala hilo, unapaswa kufuatilia sauti zenye mantiki kutoka jumuiya ya kimataifa na kutoka ndani ya Marekani, kuondoa kodi zote za upande mmoja kwa China, na kutafuta njia za kutatua migongano kwa kupitia mazungumzo ya kufanyika kwa usawa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma