China inalinda mfumo wa biashara duniani huku kukiwa na mivutano kutokana na ushuru wa Marekani, asema balozi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2025
China inalinda mfumo wa biashara duniani huku kukiwa na mivutano kutokana na ushuru wa Marekani, asema balozi
Balozi wa China nchini Uingereza Zheng Zeguang (mbele ) akitoa hotuba kwenye hafla ya kuhimiza uwekezaji na biashara kwa mji wa bandari wa Tianjin, kaskazini mwa China, iliyofanyika London, Uingereza, Aprili 24, 2025. (Xinhua/Li Ying)

LONDON – Upingaji na hatua thabiti za kulipiza za China kwa kile kinachoitwa "ushuru wa Reciprocal" wa Marekani zinalenga si tu kulinda maslahi yake ya taifa, lakini pia kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi na kudumisha haki ya kimataifa, amesema Balozi wa China nchini Uingereza Zheng Zeguang jana Alhamisi.

Balozi huyo ametoa kauli hiyo kwenye hafla ya kuhimiza uwekezaji na biashara kwa mji wa bandari wa Tianjin, kaskazini mwa China, iliyofanyika katikati mwa jiji la London.

Kile kinachoitwa "ushuru wa Reciprocal" wa Marekani uliowekwa kwa washirika wake wote wa kibiashara, zikiwemo China na Uingereza, "ni ukiukaji wa wazi wa kanuni za WTO, na kitendo cha uamuzi wa upande mmoja, kujihami na ukandamizaji wa kibiashara," amesema Balozi Zheng.

"Imetoa pigo kubwa kwa mfumo wa biashara wa pande nyingi na uchumi duniani, kudhoofisha sana maslahi ya nchi zote." ameongeza.

Balozi huyo amesema kuwa, katika kipindi cha siku chache zilizopita, Washington imekuwa ikituma ishara za kutatanisha, ikitangaza ushuru wa juu kwa baadhi ya nchi za Asia wakati huohuo ikisema kuwa zitapunguza kwa kiasi kikubwa ushuru kwa China, huenda Marekani inataka kutumia kitendo hiki kupunguza hasara yake yenyewe na kushawishi soko la mitaji.

Amesisitiza msimamo wa China kwamba kuanzia siku ya kwanza, vita vya ushuru na biashara havina washindi, akisisitiza kwamba China haitafuti vita lakini haiviogopi, na itapigana ikibidi.

Huku akisisitiza kwamba milango ya China iko wazi kama Marekani inataka kuzungumza, Balozi Zheng amesema: "Lakini kwa sasa, hakuna majadiliano yanayofanyika kati ya China na Marekani."

Ameongeza kuwa mazungumzo yoyote yanapaswa kufanyika juu ya msingi wa usawa, kuheshimiana, na kunufaishana, na ameihimiza Marekani kuachana na "shinikizo la juu zaidi, vitisho na ulaghaii."

Balozi Zheng pia ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuonesha mshikamano na kuchukua hatua pamoja dhidi ya maamuzi ya upande mmoja na ukandamizaji wa kibiashara.

"Kuridhisha au kujisalimisha kutaleta tu matatizo zaidi na kumtia moyo mkandamizaji," ameonya.

Balozi huyo pia ameelezea matumaini yake kwamba Uingereza itashikilia desturi yake ya muda mrefu ya kupigania biashara huria na ya wazi, itabaki katika upande sahihi wa historia, kuunga mkono ushirikiano wa pande nyingi na kuendana na sehemu kubwa ya jumuiya ya kimataifa juu ya suala hilo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha