

Lugha Nyingine
"Ushuru wa chini zaidi ni mzuri kwa kila mmoja": Rais wa Benki ya Dunia
Rais wa Kundi la Benki ya Dunia Ajay Banga akizungumza wakati wa Mikutano ya Majira ya mchipuko ya 2025 ya Kundi la Benki ya Dunia (WBG) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Washington, D.C., Marekani, Aprili 22, 2025. (Xinhua/Xie E)
WASHINGTON - Rais wa Kundi la Benki ya Dunia (WBG) Ajay Banga kwenye shughuli moja iliyofanyika jana Jumanne katika Mikutano ya Majira ya Mchipuko ya 2025 ya Kundi la Benki ya Dunia (WBG) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) amesema kwamba ushuru wa chini zaidi ni mzuri kwa kila mmoja, huku akisema kuwa ameshuhudia kuongezeka kwa biashara kati ya kanda na biashara ya pande mbili katika miaka ya hivi karibuni.
"Katika miaka 10 iliyopita, kama ukiangalia idadi ya mikataba ya biashara ya pande mbili na ya kikanda inayotiwa saini duniani, ni zaidi ya kile ambacho watu wengi wanakizingatia," Banga amesema.
"CPTPP, RCEP, hii yote ni mikataba inayohusisha nchi mbalimbali katika muongo uliopita, na imebadilisha namna biashara inavyofanya kazi katika nchi hizo," Banga amesema, akirejelea Mkataba Jumuishi na Maendeleo kwa Ushirikiano wa Kuvuka Pasifiki, na Ushirikiano Jumuishi wa Kiuchumi wa Kikanda - mikataba miwili mikubwa ya kibiashara katika eneo la Asia-Pasifiki.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari wiki iliyopita, rais huyo wa Benki ya Dunia alisema kuwa kuna "uwezo ambao haujatumiwa" katika ushirikiano wa kina wa kikanda.
"Biashara miongoni mwa nchi zinazoendelea inakua kwa kasi. Karibu nusu ya mauzo ya nje kutoka nchi hizi ... sasa inakwenda katika masoko mengine yanayoibukia," Banga amesema.
"Kuimarisha uhusiano wa kikanda kupitia michakato yenye ufanisi zaidi ya mipaka, gharama ya chini ya biashara, mikwaruzano michache, sheria wazi katika maeneo ya asili, haya yanaweza kuongeza kiwango cha biashara na kuunga mkono ukuaji tulivu na wenye anuai," amesema.
Rais huyo wa Benki ya Dunia pia amesema kuwa nchi nyingi zinazoendelea bado zinadumisha ushuru wa juu kuliko nchi zinazoendelea, ukiwa na ushuru wa bidhaa muhimu zilizoagizwa kutoka nje kwa asilimia kadhaa juu ya wastani, ambayo inaleta hatari halisi ya "ushuru wa Reciprocal" na kupoteza uwezo wa ushindani.
"Kwa hivyo biashara huria yenye msingi mpana, si tu na wenzi wa ushirikiano, unaweza kusaidia kukabiliana na hatari hizi na kwakweli kupanua ufikiaji wa soko," amesema, akiongeza kuwa historia inaonyesha kuwa nchi zenye uchumi ulio wazi zaidi zinaweza kukua kwa kasi na zinahimili hisa na mishtuko kwa ufanisi zaidi.
Banga amewaambia waandishi wa habari kuwa hali ya kutokuwa na uhakika na kuyumba kunasababisha katika mazingira ya tahadhari zaidi ya kiuchumi na kibiashara, akihimiza nchi kufanya mazungumzo kuhusu masuala ya biashara.
Rais wa Kundi la Benki ya Dunia Ajay Banga akihudhuria Mikutano ya Majira ya mchipuko ya 2025 ya Kundi la Benki ya Dunia (WBG) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Washington, D.C., Marekani, Aprili 22, 2025. (Xinhua/Xie E)
Rais wa Kundi la Benki ya Dunia Ajay Banga akizungumza katika Mikutano ya Majira ya mchipuko ya 2025 ya Kundi la Benki ya Dunia (WBG) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Washington, D.C., Marekani, Aprili 22, 2025. (Xinhua/Xie E)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma