

Lugha Nyingine
Rais Xi amsifu Mama Malkia Monineath kama mhimizaji wa urafiki kati ya China na Cambodia
Rais wa China Xi Jinping akikutana na Mama Malkia wa Cambodia Norodom Monineath Sihanouk katika Ikulu ya Kifalme mjini Phnom Penh, Cambodia, Aprili 17, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)
PHNOM PENH -- Rais wa China Xi Jinping katika mkutano wake na Mama Malkia katika Ikulu ya Kifalme jana Alhamisi amesema kuwa Mama Malkia wa Cambodia Norodom Monineath Sihanouk ni shahidi na mhimizaji wa urafiki kati ya China na Cambodia.
Rais Xi amesema Mama Malkia huyo ana hisia maalum za kirafiki kwa watu wa China, na anastahili vema kutunukiwa Nishani ya Urafiki ya Jamhuri ya Watu wa China.
Rais Xi pia amesema kuwa China ni maskani yake ya pili, na anakaribishwa kuja China wakati wowote.
Rais Xi amesema, Baba Mfalme wa Cambodia Norodom Sihanouk alikuwa bendera ya urafiki kati ya China na Cambodia, alikuwa pamoja na viongozi wazee wa China, yeye binafsi alianzisha urafiki imara kama chuma usioweza kuvunjika kati ya China na Cambodia.
"Tutakumbuka siku zote mchango wa kihistoria aliotoa," Rais Xi ameongeza.
Kwa upande wake, Mama Malkia amesema Rais Xi ni rafiki mkubwa wa Cambodia, na ana furaha kubwa kuona kwamba urafiki kati ya China na Cambodia ulioanzishwa na viongozi wazee wa nchi hizo mbili umekuwa ukiimarishwa na kuendelezwa siku hadi siku.
Mama Malkia amesema anaamini kwamba urafiki imara kama chuma kati ya nchi hizo mbili utaendelezwa kwa kina zaidi na usioweza kuvunjika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma