Viongozi wa Afrika waandaa njia kwa ajili ya utetezi wa haki ya fidia duniani kwenye mkutano wa Accra

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 22, 2026

Picha hii iliyopigwa Juni 19, 2026 ikionyesha mwonekano wa Ngome ya Christiansborg, kituo cha zamani cha kushikilia watumwa, Accra, Ghana. (Picha na Seth/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Juni 19, 2026 ikionyesha mwonekano wa Ngome ya Christiansborg, kituo cha zamani cha kushikilia watumwa, Accra, Ghana. (Picha na Seth/Xinhua)

ACCRA - Viongozi wa Afrika na washirika wao duniani katika utetezi wa haki ya fidia wamemaliza mkutano wao wa siku tatu huko Accra, mji mkuu wa Ghana, wakitoa njia bayana za kuhimiza kuuongezea nguvu utetezi duniani kwa ajili ya haki ya fidia.

Mkutano wa Mashauriano wa Ngazi ya Juu kuhusu utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa lenye umuhimu wa kimnara juu ya Usafirishaji Haramu wa Waafrika Waliotumikishwa Utumwani ulimalizika Ijumaa jioni baada ya kupitishwa kwa dira ya kuongoza utetezi duniani kwa ajili ya fidia ya kihistoria.

Nyaraka iliyopitishwa kwenye mkutano huo ya Hatua Zinazofuata za Accra juu ya Haki ya Fadhila, inatarajiwa kuongoza mapambano ya kujipatia haki kwa Afrika na watu wenye asili ya Afrika kwa dhuluma za kibinafsi, za kijamii, na za kihistoria walizopitia kutokana na biashara ya utumwa ya kuvuka Atlantiki, ukoloni, na ubaguzi wa rangi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana Samuel Okudzeto Ablakwa amesema, nyaraka hiyo yenye aya 46 inaelezea hatua za kivitendo za kufikia utekelezaji wa sheria kwa kujipatia haki ya fidia, inayotarajiwa katika mfumo wa kurejesha mali, kulipa fidia, ujengaji wa kijamii, mageuzi ya kitaasisi, na uhakikisho wa kutorudiwa.

Malengo makuu ni utafutaji wa ukweli wa mambo na utambuzi, haki ya kisheria, kurejeshwa kwa vitu vya mabaki ya kale ya kitamaduni, mageuzi ya usimamizi wa dunia, malipo ya fidia, haki ya kijinsia, ujengaji upya kisaikolojia, ushiriki wa watu wenye asili ya Afrika wanaoishi ng’ambo, upunguzaji wa madeni, haki ya mambo ya fedha , uhamishaji teknolojia, afya ya umma, na haki ya tabianchi.

"Athari za usafirishaji haramu wa Waafrika waliotumikishwa utumwani na unyonyaji kwa misingi ya rangi kwa watu wa Afrika havijaisha lakini vinaendelea kujidhihirisha katika hali isiyo ya usawa kwa misingi ya rangi, tofauti za maendeleo, uharibifu wa ardhi, na aina nyingine za dhuluma," Ablakwa amesema.

Moja ya matokeo muhimu ya mkutano huo ni kuimarishwa kwa juhudi za makundi kadhaa yanayohusika ya Waafrika katika kupigania haki ya fidia, ikiwa ni pamoja na kampeni ya Jumuiya ya Karibeani (CARICOM), kampeni ya Wamarekani Waafrika, na kampeni ya Umoja wa Afrika (AU).

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Fidia ya CARICOM Hilary Beckles amesema kwenye mkutano huo kwamba mpango wa CARICOM wa pointi 10 wa haki ya fidia sasa ni sehemu ya "Uelewa wa Waafrika duniani."

Wajumbe wa Mkutano wa Mashauriano wa Ngazi ya Juu kuhusu utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa lenye umuhimu wa kimnara juu ya Usafirishaji Haramu wa Waafrika Waliotumikishwa Utumwani wakitembelea Ngome ya Christiansborg, kituo cha zamani cha kushikilia watumwa, huko Accra, Ghana, Juni 19, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

Wajumbe wa Mkutano wa Mashauriano wa Ngazi ya Juu kuhusu utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa lenye umuhimu wa kimnara juu ya Usafirishaji Haramu wa Waafrika Waliotumikishwa Utumwani wakitembelea Ngome ya Christiansborg, kituo cha zamani cha kushikilia watumwa, huko Accra, Ghana, Juni 19, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha