Rais Xi asisitiza maendeleo yenye uwiano kati ya maeneo na kuhimiza ustawi wa pamoja kwa hatua madhubuti

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 18, 2026

BEIJING - Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amehimiza juhudi zaidi za kusukuma mbele maendeleo yenye uwiano kati ya maeneo toauti, na kuhakikisha juhudi za kuhimiza ustawi wa pamoja wa watu wote zinapata maendeleo kwa hatua zinazotekelezwa kihalisi.

Xi, ameyasema hayo katika maagizo ya hivi karibuni juu ya kusukuma mbele kwa hatua madhubuti ushirikiano kati ya maeneo ya mashariki na magharibi mwa China.

"Katika miaka 30 iliyopita, ushirikiano kati ya maeneo ya mashariki na magharibi umefanya kazi kubwa katika kusaidia kushinda mapambano dhidi ya umaskini na kusukuma mbele maendeleo yenye uwiano kati ya maeneo tofauti,” Xi amesema.

Xi akisema kuwa mwaka 2026 ni mwaka wa kwanza wa kutekeleza utaratibu wa kutoa msaada wa hali ya kawaida, na ametoa wito wa kujifunza na kutumia uzoefu muhimu uliopatikana kutoka kwenye ushirikiano kati ya Mkoa wa Fujian mashariki mwa China na Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wahui wa Ningxia kaskazini magharibi, kukamilisha utaratibu wa ushirikiano, na kupanua wigo wa ushirikiano.

“Ni muhimu sana kuhimiza maeneo tofuati kusaidiana katika viwanda, mabadilishano ya wafanyakazi, kufundishana katika teknolojia, kubadilishana mawazo, na kufunzana mienendo ya kufanya kazi, ili kufanya ushirikiano wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja,” Xi amesema.

Amesema kamati za chama na serikali katika ngazi zote zinapaswa kutimiza kwa makini wajibu wao wa utoaji msaada wa hali ya kawaida, kuzuia kithabiti idadi kubwa ya watu waliopunguza hali ya umaskini wasikabiliwe tena na umaskini au kuongezeka kwa watu wenye hali ya umaskini, na kujipatia maendeleo kwa hatua halisi katika kusukuma mbele ustawi wa vijiji katika pande zote. 

Maagizo hayo ya Xi yametolewa kwenye mkutano wa kitaifa kuhusu ushirikiano kati ya maeneo ya mashariki na magharibi mwa China uliofanyika jana Jumatano mjini Yinchuan, Ningxia.

Liu Guozhong, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na naibu waziri mkuu wa China, alihudhuria mkutano huo.

Liu amesisitiza kuwa ni lazima kuwa na wazo sahihi kuhusu “kufanya mambo mazuri” na kulitekeleza, kuzidisha ushirikiano wa viwanda na ushirikiano wa huduma za wafanyakazi kati ya maeneo ya Mashariki na Magharibi mwa China, kuimarisha mabadilishano ya maofisa na wataalamu, na kupanua ushirikiano katika sekta ya sayansi, teknolojia na mambo ya fedha. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha