Lugha Nyingine
Watu zaidi ya 200 wafariki kutokana na mvua kubwa na mafuriko kusini mwa Afrika
Wiki za mvua kubwa mfululizo na mafuriko katika maeneo mengi vimeathiri nchi kadhaa za kusini mwa Afrika ikiwemo Afrika Kusini, Msumbiji na Zimbabwe, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 200, kuharibu mali na kusababisha operesheni kubwa za kuhamisha na kuokoa watu.
Kituo cha Kitaifa cha Kusimamia Maafa cha Afrika Kusini jana jumapili kimetangaza janga la kitaifa kutokana na mvua kubwa na mafuriko kuendelea kuathiri maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo.
Nchini Msumbiji, takwimu zilizotolewa Ijumaa mwishoni mwa wiki iliyoisha na Taasisi ya Kitaifa ya Usimamizi wa Maafa na Kupunguza Hatari zimeonyesha kuwa, watu karibu 103 wamefariki kufuatia msimu usio wa kawaida wa mvua, huku watu wengine zaidi ya 200,000 wakiathirika na mvua hizo nchini humo.
Wakati huohuo, nchini Zimbabwe, Idara ya Ulinzi wa Raia nchini humo imesema, watu 70 wamefariki na nyumba zaidi ya 1,000 zimebomolewa tangu mwanzoni mwa mwezi huu, huku shule, barabara na madaraja yakiharibiwa ama kusombwa na mafuriko.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



