Jeshi la Somalia lazuia shambulizi dhidi ya kambi ya jeshi

(CRI Online) Januari 19, 2026

Jeshi la Somalia limezuia shambulizi lililofanywa na wapiganaji wa kundi la al-Shabab dhidi ya kambi ya jeshi katika eneo la kusini-kati mwa nchi hiyo hapo jana Jumapili.

Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo imesema, operesheni kubwa inayohusisha upelelezi na vikosi vya usalama inaendelea ili kuangamiza wapiganaji wowote waliosalia katika eneo la Jabad Godane, kuwazuia kujikusanya upya, na kuhakikisha usalama kwa jamii za wenyeji.

Kundi la Al-Shabab, ambalo linataka kuipindua serikali ya Somalia inayotambulika kimataifa, limedai kuhusika na mashambulizi katika kambi nne za jeshi karibu na wilaya ya Warsheikh, ambapo askari 21 waliuawa, wengine 11 kujeruhiwa, na kuteka magari ya kijeshi na silaha.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha