Bandari ya Biashara Huria ya Hainan laanza uendeshaji maalum wa forodha kisiwani kote: Ukurasa mpya katika kufungua mlango

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 19, 2025

Bandari ya Biashara Huria ya Hainan ya China (FTP) imeanza rasmi uendeshaji maalum wa forodha kisiwani kote jana Alhamisi Desemba 18, ikimaanisha hatua kubwa kuelekea ufunguaji mlango wa ngazi ya juu zaidi.

Chini ya mfumo huo mpya wa forodha, mkoa huo wa kisiwa wa Hainan kusini mwa China utafanya kazi kama eneo la forodha linalojitegemea kiasi lenye mundo maalum wa usimamizi unaoelezewa kuwa ni "ufikiaji huria zaidi kwenye mstari wa kwanza, ufikiaji uliodhibitiwa kwenye mstari wa pili, na mtiririko huria ndani ya kisiwa hicho."

"Mstari wa kwanza" unarejelea uunganisho wa Hainan na masoko ya nje ya nchi, huku "mstari wa pili" ukirejelea mpaka wa forodha kati ya Hainan na sehemu nyingine za China bara, kwa mujibu wa maafisa husika.

Rais wa China Xi Jinping alitangaza uamuzi wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) wa kuunga mkono kuiendeleza Hainan kuwa eneo la majaribio la biashara huria na kuiunga mkono Hainan kutafuta njia na kusongeza mbele kwa hatua madhubuti ujenzi wa bandari ya biahara huria yenye umaalum wa China mwezi Aprili 2018, kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Mkoa wa Hainan na Eneo Maalum la Kiuchumi la Hainan.

“Lengo hilo la kimkakati la kujenga Bandari ya Biashara Huria ya Hainan ni kuifanya kuwa lango muhimu linalochochea ufunguaji mlango wa China katika zama mpya,” Rais Xi alisema kwenye mkutano wa hivi karibuni juu ya Bandari ya Biashara Huria ya Hainan.

Uendeshaji maalum wa forodha wa kisiwani kote ni mpangilio muhimu uliowekwa kwenye mpango wa jumla wa ujenzi wa Bandari ya Biashara Huria ya Hainan, uliotolewa na serikali kuu mwaka 2020.

Hii ni hatua muhimu katika ujenzi wa FTP ya Hainan, kwa mujibu wa Zhou Mi, naibu mkuu wa Taasisi ya Masomo ya Amerika na Oceania ya Akademia ya Biashara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Kiuchumi ya China chini ya Wizara ya Biashara ya China.

“Hatua hiyo inabeba umuhimu wa kimsingi kwa ajili ya kuvutia rasilimali zenye ubora duniani kwa Hainan na kuunga mkono maendeleo yanayoendeshwa na uvumbuzi ya mkoa huo,” Zhou amesema, akibainisha kuwa itaongeza kwa kiasi kikubwa nguvu hai ya soko.

Ukipatikana kwenye makutano ya Bahari za Pasifiki na Hindi, na kuungwa mkono na soko kubwa la ndani la China, Mkoa wa Hainan unafurahia faida bora za mazingira katika kuunganisha masoko duniani, hasa yale ya Asia Kusini-Mashariki.

Ukichukua uendeshaji huo maalum wa forodha wa kisiwa hicho kama fursa, mkoa huo wa Hainan unapanua ufunguaji wa kitaasisi kwa kasi tulivu, ukihimiza zaidi mtiririko huria wa bidhaa na mambo mengine, kuanzisha utaratibu wa vipaji wenye ufunguaji mlango zaidi, na kuzidisha mageuzi ya kazi za serikali, yote yakilenga kusukuma mbele maendeleo yenye sifa bora ya Bandari ya Biashara Huria ya Hainan.

Bustani ya Viwanda vya Intaneti mjini Haikou, mji mkuu wa Mkoa wa Hainan, sasa ni mwenyeji wa kampuni zaidi ya 10,000, huku mapato ya jumla yakizidi yuan bilioni 160 (dola za Marekani bilioni 22.7) mwaka 2024, kwa mujibu wa Wu Qingji, meneja mkuu wa bustani hiyo ya viwanda.

“Viwango vya chini vya kodi, mifumo ya kodi iliyorahisishwa na sera za ushuru-sifuri za Bandari ya Biashara Huria ya Hainan vimepunguza kwa kiasi kikubwa gharama za uendeshaji kwa kampuni,” Wu amesema.

Matumizi yasiyotozwa ushuru pia yanatarajiwa kunufaika. Kufuatia uzinduzi rasmi wa uendeshaji huo maalum wa forodha kisiwani kote, idadi ya kategoria za bidhaa zisizotozwa ushuru zitapanuka kutoka takriban 1,900 hadi takriban 6,600, ikiwezesha wadau wengi zaidi wa soko kunufaika na sera ya ushuru-sifuri.

Feng Chonghan, naibu meneja mkuu wa Eneo la Kimataifa la Maduka Mengi Yasiyotozwa Ushuru la Sanya mjini Sanya, Hainan, amesema mfumo huo mpya wa forodha utaleta uwezekano usio na kikomo kwenye eneo hilo la ununuzi, kwa kupunguza gharama za ununuzi, kuongeza utoaji wa bidhaa, na kuboresha mifumo ya biashara.

“Kwa utekelezaji kamili wa sera za upendeleo kwa Bandari ya Biashara Huria ya Hainan na maeneo jumuishi ya majaribio kwa biashara ya mtandaoni ya kuvuka mipaka kote kisiwani, kampuni zinazojihusisha na biashara ya mtandaoni ya kuvuka mipaka zitashuhudia gharama za kodi zilizopunguzwa sana na ufanisi wa uchukuzi ulioboreshwa sana,” amesema Li Mingtao, mtaalamu mkuu wa biashara ya mtandaoni wa Kituo cha Biashara ya Kimataifa ya Mambo ya Kielektroniki cha China.

Gati la Kimataifa la Kontena la Yangpu huko Danzhou, Hainan, limefungua njia 59 za usafirishaji wa ndani na nje ya nchi, likiunda mtandao ambao unaunganisha masoko ya karibu na ya mbali.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Haikou Meilan mjini Haikou umeanzisha taratibu zilizorahisishwa za uidhinishaji mizigo, na kupunguza muda wa kuainisha bidhaa za forodha hadi dakika tano.

Uendeshaji maalum wa forodha pia unatarajiwa kuharakisha mtiririko wa kuingia ndani wa vipaji na rasilimali.

Lin Guangming, mtaalamu mkuu wa mpangilio wa kamati ya usimamizi ya Eneo Maalum la Maendeleo ya Kiuchumi la Yangpu la Hainan, ni mmoja wa wataalamu wa kigeni waliohusika sana katika ujenzi wa Bandari ya Biashara Huria ya Hainan.

Ameshuhudia namna Eneo hilo lilivyoibuka hatua kwa hatua kuwa mfano wa Bandari ya Biashara Huria ya Hainan.

"Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, tulikuwa 'tunaweka misingi,'" Lin amesema, akibainisha kuwa kwa kuwa uendeshaji maalum wa forodha umeanzishwa rasmi, gawio kutoka sera litatolewa haraka zaidi, na kuvutia vipaji zaidi vya kimataifa mkoani Hainan.

Katika huduma ya afya, sera za kuingia bila visa na taratibu zilizorahisishwa za kuidhinisha zimewezesha ushirikiano wa kina wa kimataifa, ikiruhusu Hospitali ya Umma ya Haikou kushirikiana na madaktari nchini Australia na Marekani, na kusaidia hospitali zaidi kuanzisha vituo vya matibabu vya kimataifa na mifumo ya huduma ya afya inayotegemea madaktari wa magonjwa yote (GP).

“Hadi kufikia Novemba 2025, Eneo la Majaribio ya Utalii wa Matibabu la Boao Lecheng mkoani Hainan lilikuwa limeshaanzisha dawa na vifaa tiba vya kivumbuzi zaidi ya 520 na kuvitumia kwa mara ya kwanza nchini China, vikinufaisha wagonjwa zaidi ya 200,000,” amesema Fu Zhu, naibu mkuu wa eneo hilo la majaribio.

“Huku uendeshaji huo maalum wa forodha ukiruhusu ‘ufikiaji huria zaidi kwenye mstari wa kwanza,’ eneo hilo la majaribio litafurahia muunganisho bora na soko la kimataifa,” Fu amebainisha.

“Kufuatia uzinduzi wa uendeshaji huo maalum wa forodha, uidhinishaji vibali vya forodha kwa dawa na vifaa tiba vinavyohitajika haraka kutoka nje kwa matumizi ya kliniki utakuwa na ufanisi zaidi,” Fu amesema.

“Sera zikiwemo za kuingia na kutoka kwa urahisi zaidi kwa wafanyakazi, kuingia bila visa kwa raia wa nchi 86, na mchakato mfupi wa idhini - unaochukua siku chache kama 15 kwa madaktari wa kigeni kuruhusiwa kufanya kazi katika Eneo la Majaribio ya Utalii wa Matibabu la Boao Lecheng - zitaunda mazingira mazuri ambayo hayajawahi kutokea kwa wagonjwa wa kimataifa na wataalamu wa matibabu wa kiwango cha juu,”alisema Fu.

Kwa mujibu wa mpango wa jumla wa ujenzi wa Bandari ya Biashara Huria ya Hainan, China inalenga kwanza kuanzisha sera ya bandari huria ya biashara na mfumo wa kitaasisi, ambao unajikita katika uhuria wa biashara na uwekezaji, pamoja na uwezeshaji ifikapo mwaka 2025, na kuuendeleza mkoa huo kuwa uchumi wenye ngazi mpya ya ufunguaji mlango ifikapo mwaka 2035 na bandari ya biashara huria ya ngazi ya juu yenye ushawishi wa kimataifa ifikapo katikati ya karne.

"Mkoa wa Hainan si tu ni lango la ufunguaji mlango wa China na uwanja wa majaribio kwa ajili ya uvumbuzi katika ufunguaji mlango, lakini pia ni dirisha ambalo kupitia kwake dunia inaweza kupata uelewa bora wa ufunguaji mlango wa China," amesema Chen Bo, mtafiti mkuu katika Chuo Kikuu cha Hainan.

"Kadri changamoto za kimataifa zinavyoendelea, Bandari ya Biashara Huria ya Hainan inatoa nafasi mpya kwa China na jumuiya ya kimataifa kuchunguza fursa za pamoja za maendeleo na njia za kivumbuzi za maendeleo," Zhou amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha